Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII



Na mwandishi wetu, Njombe

Katibu Mkuu wa Wizara ya habari, Utamaduni, sanaa na michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania amesema kwa bahati mbaya wanaowaponza na kuwarubuni Vijana na kuwaingiza kwenye uvunjifu wa sheria ya Mtandaoni wamekuwa wakiwafuata Vijana kutoka familia duni, suala ambalo limekuwa likizigharimu familia nyingi maskini kuweza kumudu uendashaji wa kesi, akihimiza Vijana kutumia vyema mitandao ya kijamii ili kutojikuta katika mikono ya sheria.

Msigwa amebainisha hayo leo Alhamisi Mei 07, 2026 wakati wa ufungzi wa Kikao kazi cha 21 cha Maafisa habari, mawasiliano, itifaki na uhusiano serikalini, kinachofanyika Mjini Njombe, Kusini Magharibi mwa Tanzania, akihimiza Vijana kujiepusha na matukio ya kufuata mkumbo ama kurubuniwa na baadhi ya wanaharakati wanaovunja sheria za nchi na kutoitakia mema Tanzania.

"Mimi huwa nakutakanwa sana kwenye mitandao ya kijamii na ninawaambia msinitukane mtapatikana, hawanisikii leo Polisi imekusanya wengi na mule ndani kuna watoto wa maskini kisa tu kaamasishwa. Leo teknolojia ilipofika huwezi ukatukana mtandaoni ukabaki salama, lazima utashikwa. Na bahati mbaya wanaowapotosha Vijana wanatafuta Vijana ambao wanatoka familia duni. Ukifanya uhalifu utakamatwa ukiwa ni mtumishi wa umma ama ukiwa si mtumishi wa umma utapatikana." Amesema Bw. Msigwa.

Kiongozi huyo pia katika hatua nyingine amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii nchini, akiwataka pia vijana kujiepusha na mikumbo kwani asilimia kubwa ya wanaohamasisha vijana kuvunja sheria za nchi hawapo nchini na pale hatua za kisheria zinapochukuliwa waathirika wakubwa wamekuwa ni watoto na Vijana wa kitanzania wanaotokea familia duni zisizokuwa na uwezo wa kusimamia kesi mahakamani dhidi ya Vijana wao waliovunja sheria kwa hamasa kutoka nje ya Nchi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com