Mwanafunzi Joenice Jeremiah, mmoja wa washiriki wa timu ya Savannah Plains, akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani. Picha na Kadama Malunde

Afisa kutoka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Albert Kingu, akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi wa Savannah Plains waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.
Mkuu wa Shule ya Savannah Plains, Josephine Kinyunyi, akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.
WANAFUNZI SAVANNAH PLAINS WAENDA KENYA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MJADALA
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, wameelekea jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa Shule za Afrika Mashariki kwa Lugha ya Kiingereza (East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2026).
Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Mei 7 hadi 11, 2026, yakitarajiwa kuwakutanisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki na maeneo mengine ya bara la Afrika.
Katika mashindano hayo, Savannah Plains inawakilishwa na timu ya wanafunzi 21 kutoka kidato cha kwanza hadi cha tatu, waliokwenda kuonyesha uwezo wao katika mjadala, hotuba na mawasiliano ya hadhara kwa kiwango cha kimataifa.
Akizungumza leo Mei 6, 2026, Mkuu wa Shule hiyo, Josephine Kinyunyi, amesema shule imejiandaa kikamilifu kwa mashindano hayo na ina matumaini makubwa ya kurejea nyumbani ikiwa na medali pamoja na makombe.
Amesema wanafunzi wa Savannah Plains wamejengewa misingi imara ya maadili, taaluma na ujuzi wa kujieleza, jambo litakalowasaidia kushindana kwa kujiamini kwenye majukwaa ya kimataifa.
“Tunakwenda kuitangaza Tanzania na kuonyesha uwezo wa wanafunzi wetu katika ramani ya dunia,” amesema Kinyunyi.
Afisa kutoka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Albert Kingu amesema idara hiyo imeendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa kuhakikisha taratibu zote muhimu za safari zinakamilishwa kwa wakati, ikiwemo huduma za hati za kusafiria, ushauri wa masuala ya mipakani pamoja na kuwaelekeza wanafunzi na walimu kuhusu sheria za usafiri wa kimataifa, ili kuwawezesha kushiriki mashindano hayo kwa utulivu na mafanikio.
Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Shinyanga, Richard Makoye, ameipongeza Shule ya Sekondari Savannah Plains kwa hatua ya kuwapeleka wanafunzi kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani nchini Kenya, akisema ni ishara ya ubora wa elimu inayotolewa shuleni hapo.
Amesema ushiriki huo unawajengea wanafunzi kujiamini, uwezo wa mawasiliano, ushindani wa kimataifa na kuitangaza vyema Shinyanga pamoja na Tanzania.
Aidha, amewataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kujifunza, kufanya vizuri na kurejea na ushindi pamoja na uzoefu utakaowanufaisha katika masomo na maisha yao ya baadaye.
Mratibu wa Somo la Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains, Jackson Karani, ambaye pia ni kiongozi wa msafara wa timu hiyo, amesema wanafunzi wamejiandaa kikamilifu kushiriki mashindano hayo na wana ari kubwa ya kufanya vizuri.Amesema maandalizi yaliyofanyika kwa muda mrefu yamewajengea uwezo wa kujieleza kwa kujiamini, kushindana kwa nidhamu na kuiwakilisha vyema Savannah Plains pamoja na Tanzania katika jukwaa la kimataifa.
Kwa upande wao, wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo akiwemo Collins Mashaka na Joenice Jeremiah wamesema wamejiandaa kikamilifu kupitia mazoezi ya mijadala, hotuba za hadhara, kuongeza uwezo wa lugha ya Kiingereza pamoja na kujifunza mbinu za ushindani wa kimataifa, wakieleza kuwa lengo lao ni kufanya vizuri, kurudi na ushindi pamoja na kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Savannah Plains ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma na katika shughuli za kukuza vipaji vya wanafunzi. Shule hiyo ya bweni ipo Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, mkabala na barabara kuu ya Shinyanga kuelekea Mwanza.
Pia taasisi hiyo ina Savannah Plains High School inayotoa michepuo mbalimbali ikiwemo PCM, PCB, PGM, HGE, EGM, HGL, HGK, HKL na ECA.
Afisa kutoka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Albert Kingu, akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi wa Savannah Plains waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.
Afisa kutoka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Albert Kingu, akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi wa Savannah Plains waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi, akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.
Mwanafunzi Collins Mashaka, mmoja wa washiriki wa timu ya Savannah Plains, akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi, akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi waliokuwa wakielekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya kimataifa ya mjadala na kuongea hadharani.

























Social Plugin