
Mume wa marehemu Victory Emmanuel Senge, Bw. Victor, akishiriki kushusha jeneza lenye mwili wa mkewe wakati wa mazishi yaliyofanyika Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mume wa marehemu Victory Emmanuel Senge, Bw. Victor, akiweka udongo katika kaburi la mkewe wakati wa maziko yaliyofanyika Mjini Shinyanga.

Mume wa marehemu Victory Emmanuel Senge, Bw. Victor, akiweka shada la maua katika kaburi la mkewe wakati wa mazishi yaliyofanyika Mjini Shinyanga.
Baba mzazi wa marehemu Victory Emmanuel Senge, Mchungaji Emmanuel Senge, akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya binti yake iliyofanyika Mjini Shinyanga.
Baba mzazi wa marehemu Victory Emmanuel Senge, Mchungaji Emmanuel Senge, akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya binti yake iliyofanyika Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Victory Emmanuel Senge wakati wa shughuli za mazishi zilizofanyika Mjini Shinyanga.

Victory Emmanuel Senge enzi za uhai wake

Victory Emmanuel Senge enzi za uhai wake
Victory Emmanuel Senge enzi za uhai wake
Mamia ya waombolezaji wamejitokeza kushiriki mazishi ya marehemu Victory Emmanuel Senge (35) yaliyofanyika Mjini Shinyanga, kufuatia kifo chake kilichotokea Jumamosi Mei 2, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya changamoto za uzazi.
Ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzake pamoja na wakazi wa Shinyanga wamejitokeza kwa wingi katika eneo la Bushushu, Mwalugoye, leo Jumatano Mei 6, 2026 kushiriki ibada ya kumuaga na safari ya mwisho ya marehemu ambaye alikuwa akiheshimika kwa wengi kutokana na utu wake na mchango wake kwa jamii.
Marehemu Victory alikuwa Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, ambapo alihudumu kwa weledi mkubwa na kujenga mahusiano mazuri na wateja pamoja na jamii kwa ujumla.
Mbali na kazi yake serikalini, marehemu pia alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa na mmiliki wa maduka ya nguo ya Victorious yaliyopo Ngokolo Mjini Shinyanga, jambo lililomfanya kugusa maisha ya watu wengi kupitia ajira na huduma zake.
Ibada ya kuaga mwili ilianza nyumbani Mwalugoye kabla ya kuendelea katika Kanisa la TAG PCC Bushushu, ambako waombolezaji walipata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho na kumuombea marehemu.
Baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu ulisindikizwa kwenda makaburini Bushushu yaliyopo Barabara ya Shy Park ambako ulizikwa huku simanzi na huzuni vikitawala kwa waombolezaji wengi waliohudhuria.
Wengi waliomfahamu wameeleza kushtushwa na kifo chake, wakimtaja kuwa alikuwa mtu mwenye upendo, mchapakazi, mwenye moyo wa kusaidia na aliyekuwa karibu na jamii.
Kifo cha Victory Senge kimeacha pengo kubwa kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na jamii ya Shinyanga kwa ujumla, huku akikumbukwa kwa uchapakazi wake, moyo wa kujituma na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii.
Mwili wa Victory Emmanuel Senge ukitolewa nyumbani kwake Bushushu Mjini Shinyanga kwa ajili ya kupelekwa Kanisani

Mwili wa Victory Emmanuel Senge ukiwasili Kanisani
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog































































































































Social Plugin