Showing posts with label utamaduni lake zone. Show all posts
Showing posts with label utamaduni lake zone. Show all posts

Monday, January 19, 2015

ANGALIA PICHA_MSANII BHUDAGALA MWANAMALONJA AKUSANYA MAELFU YA WAKAZI WA GEITA KATIKA SHOW YAKE

Hapa ni katika viwanja vya mji wa Kasamwa mkoani Geita ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita msanii wa nyimbo za asili Kutoka kanda ya ziwa Victoria Bhudagala Mwanamalonja aliangusha show/burudani babu kubwaa katika kuukaribisha mwaka mpya 2015 na wakazi wa Geita.Maelfu ya watu kutoka kila kona ya mkoa wa Geita walijitokeza.
Share:

Sunday, January 18, 2015

TAZAMA VIDEO YA KAKA JAY- Wimbo Unaitwa "TANZANIA"


Tazama  Video ya Joash Timothy Omolo maarufu kwa jina la "Kaka Jay" kutoka Kahama,mkoa wa Shinyanga,nchini Tanzania,wimbo unaitwa "Tanzania"
Share:

Saturday, December 27, 2014

BHUDAGALA NOMA SANA!!! TAZAMA VIDEO YAKE MPYA KAIACHIA INAITWA "NYABHULUGUTU"

 Msanii maarufu wa nyimbo za asili kutoka Kanda ya Ziwa Bhudagala Mwanamalonja ameachia  video ya wimbo wake unaitwa Nyabhulugutu.Itazame hapa bila shaka weekend yako itakwenda vizuri
Share:

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU GAMBOSHI- SEHEMU YA MWISHO

 
Share:

Monday, December 15, 2014

ANGALIA PICHA_ HAIJAWAHI KUTOKEA,WASANII MAARUFU WA NYIMBO ZA ASILI BHUDAGALA MWANAMALONJA NA MCHELE MCHELE WAKUTANA LIVEE!!

Haijawahi kutokea Kanda ya Ziwa ndiyo maneno yaliyotawala leo katika eneo la Kisesa Mkoani Mwanza.Mapema leo wasanii maarufu/waimbaji wa nyimbo za asili hususani kabila la Kisukuma maarufu sana katika kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla leo wamekutana kila mmoja na kundi lake. Bhudagala Mwanamalonja na kikundi chake kutoka Serengeti mkoa wa Mara mapema leo asubuhi alimtembelea msanii mwenzake  Mchelemchele anayeishi Kisesa mkoani Mwanza.
Share:

Saturday, December 6, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 11Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya KUMI NA MOJA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
Share:

Saturday, November 22, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 9


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya TISA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 9

 MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
 timotheomathias0@gmail.com

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa

Ilipoishia.......................

Vijana wengine watano waliletwa katikati tukawa vijana sita, na mbele yetu vikakeletwa nyungo sita. Mchawi mmoja alikuja akiwa amebeba visigino vya binadamu na kuanza kutugawia kila mmoja wetu alienea.
Kisigino kilikuwa kibichi kilionekana kimetoka kukatwa muda si mrefu kutoka kwa binadamu.

Mkuu wa wachawi alianza kutuelekeza na kutupa masharti alisema, kisigino ndiyo rimoti yenu, pia na matumizi yake alituelekeza.

Alitusisitiza kuwa tusipite karibu na kanisa la aina yoyote.
Kila mmoja wetu alikaa kwenye ungo wake tayari kwa safari ya kwenda Nigeria.....
Endelea ...........

Tukiwa tumekaa tayari kwa ajiri ya safari, bibi aliyetugawia nyungo alikuja kwa haraka sana akiwa anahema sana na kuanza kusema:

 "Wasiondoke kwanza maana hawajafanya tambiko la mwisho"
Katika sehemu tuliyokuwa tumekaa watu wote walikaa kimya ili kumsikiliza bibi anachozungumza. 
Mchawi mmoja wa kizungu alichomoka kutoka katikati, mkononi akiwa ameshikilia panga kali sana, alienda moja kwa moja mpaka sehemu alikokuwa amesimama yule bibi.
Bibi alikuwa na nywele ndefu sana kichwani,mzungu alipofika kwa bibi alishika nywele za bibi na panga lake lilitua shingoni mwa bibi na kukitenganisha kiwiliwili na kichwa.

Maeneo tuliyokuwa tumekaa yalitapakaa damu ya bibi aliyekatwa panga na mchawi mzungu.
Mpenzi msomaji wa stori hii, kwa macho yangu sikuweza kuamini nilichokiona machoni mwangu, baada bibi huyo kutenganishwa kiwiliwili na kichwa nilishangaa kuona kiwiliwili kubaki kimesimama takribani dakika mbili na pia kiliweza kutembea hatua tatu baadaye kilianguka na kuanza kudundadunda takribani dakika 6 baadae kilitulia tuli.
Upande wa kichwa alibaki nacho mzungu na kuanza kunywa damu.

Damu ilipoganda kichwa alikitupa chini karibu na kiwiliwili, visigino na mikono ya bibi vilikatwa na bibi alibebwa na kwenda kupikwa kwa ajili ya msosi.
Mzungu alipomaliza aligeukia upande wetu na watu wote walipiga makofi ishara ya kumshuru lakini mimi nilivyokuwa kauzu sikupiga makofi nilibaki namtumbulia mimacho tu.

 Mdomo wake ulitapakaa damu mpaka nguo aliyokuwa amevaa.
Kumbe kipindi sikumpigia makofi aliniona, alichokifanya alikuja moja kwa moja sehemu niliyokuwa nimekaa.
 Aliponisogelea nilihisi kama shoti ya umeme imetokea mwilini mwangu ,maana nilirushwa juu kwa kasi ya ajabu nikarudi chini na kufikia kichwa na kusimama harakaharaka na kuanza kupiga makofi kama chizi.

*****************
Baada ya hapo tulikwenda njia panda kuu ya Tanzania kwa ajili ya tambiko la mwisho, nikiwa kwenye usafiri wangu binafsi (ungo) na rimoti ya kisigino chako cha mguu nilitua taratibu njia panda na kujumuika na wengine.

Wakati  tunafanya tambiko pale njia panda, basi la aina yoyote lenye abiria lazima sehemu hiyo likifika lipate ajali na damu za abiria tunatumia wakati huo huo.

Kama gari la abiria halitatokea kwa wakati basi ujue kuna watu spesho kwa ajili ya damu.
Tukiwa katikati ya njia panda watu sita tulioteuliwa kwenda Nigeria tuliwekwa kati na kuambiwa tukae ikiwa wao wamesimama.

Mmoja wao alikuja na kuanza kutugawia mabakuli yaliyojaa damu za watu.
Baada ya hapo tukaletewa nyama za binadamu mbichi nikiwa zinatoa damu.

Hakuna ubishi tulikula na kunywa damu mpaka tukamaliza.
Tulipomaliza kula na kunywa tuliambiwa na kuahidiwa kuwa atakayekuwa wa kwanza kufika atapewa zawadi.

Unaambiwa kutoka Tanzania mpaka Nigeria unatakiwa ufike ndani ya dakika 6, maana nyungo zimesetiwa hivyo, ukizidisha dakika 6 wewe itakuwa halali ya wananchi kutoka duniani.
Kipindi hicho mkojo ulikuwa umenibana sana ilinibidi nichomoke kimya kimya kwa kitendo cha haraka nilijificha nyuma ya msitu na kuanza kukojoa. 

Nihisi kama kuna kitu kwa nyuma kinanigusa taratibu shingo niligeuka nilishtuka baada ya kumuona babu aliyegeuzwa kuwa kuku na mkuu wa wachawi yupo nyuma yangu,Duh nilitoa macho kama chura kabanwa mlango....
Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com
Share:

Saturday, November 15, 2014

Utamaduni Lake Zone_SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA NANE


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya NANE  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
Share:

Saturday, November 8, 2014

Utamaduni Lake Zone_SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 7
Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya SABA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
Share:

Saturday, November 1, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 6


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya SITA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu GamboshiSIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 6

 MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
 timotheomathias0@gmail.com

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa

Ilipoishia...........................
Kuna siku nikiwa nimekaa nimejiinamia nikiwaza yote yaliyotokea mkuu wa wachawi alinifuata na kunishika mkono na wote tukaanza kurudi kambini.
Tulipofika Sheila aliitwa na bibi mmoja pia na yeye aliitwa kwa mkuu, mkuu alimwambia bibi kuwa mwezi ujao ni sikukuu itakayofanyika nchini Nigeria, na huko zinahitajika nyama laini kama wanafunzi wa shule za msingi na baadhi ya walimu wao.
Nimekuchagulia vijana shupavu na imara utawatumia katika mashule huko vijijini kuleta wanafunzi.

Mkuu alipomaliza alitukabidhi mabegi yaliyosheheni pipi, biskuti na hela za sarafu, tayari kwa safari kwenda kuleta roho za watu kama tulivyoagizwa.
Endelea sasa...............
Safari tuliianza kuelekea mashuleni hasa shule za vijijini, katika safari yetu tulikuwa watatu mimi na Sheila tukiwa tumebeba mabegi mgongoni.
Mbali na Sheila pia tulikuwa na bibi ambaye yeye aliteuliwa na mkuu kama kiongozi wetu lakini yeye alikuwa amening'iniza mfuko wa rambo mkononi.
Kipindi hicho cheo changu kiliianza kupanda hapo GAMBOSHI kwani tuliweza kukabidhiwa gari aina ya VX land cruiser nyeusi.
Safari yetu ilianza ikiwa bibi na dreva walikaa mbele ya gari, pia na sisi tulikuwa nyuma yao.
Kwa binadamu wa kawaida hawezi kuiona safari yetu ikiwemo gari, kwani barabara zetu zipo tofauti na barabara za kawaida .
Barabara zetu ni za kishirikina zaidi, kwani zinapenya/zinapita sehemu yoyote mfano, majini, mlimami, juu ya nyumba na pia gari yetu inauwezo wa kuingia ndani ya nyumba kupitia mlangoni.

Kila kijiji lazima kuna mwanachama wa wachawi, safari yetu tuliweza kufikia tamati kijiji tulichokisudia na tulifikia kwa mwachana wetu.


"Mpenzi msomaji wa simulizi  hii kaa ukitambua fika ya kuwa CHAKULA KIKUU CHA WACHAWI NI NYAMA IKIWEMO NA YA BINADAMU"
Kweli tuliweza kufika na kukaribishwa vizuri, pia kwa macho ya kawaida tulionekana isipokuwa gari. 

Mama wa familia akiwa na mume wake na watoto watatu walitukaribisha, upande wa mume alikuwa hajui chochote mambo ya kishirikina na pia alikuwa mchungaji wa kanisa.

Mama aliweza kututambulisha kwa mume wake, na mume wake alitukaribisha kwa furaha maana alimpenda sana mungu.
Baada ya hapo mama alitupeleka katika chumba cha wageni na kutuambia kuwa tukae kwa siku tatu, ya nne tuanze kazi iliyotupeleka.
Usiku ulipofika mama alituambia kuwa nyama ya kula kesho imeisha, kwa hivyo nilitakiwa kuamka usiku kwenda kuchukua nyama.
Kweli ilipofika usiku mama alikuja kuniamsha na kuniambia tuondoke haraka,lakini kabla hatujaondoka nilimuuliza vipi kuhusu mme wako?.
Mama alionekana kushtuka kidogo na kuniambia turudi chumbani kwake.
Tuiingia taratibu mpaka kitandani na kumkuta mme wake amelala, tulichokifanya mama alichukua dawa na kumuwekea mme wake puani.
Loo!! mume alipiga chafya na kugeukia upande wa pili na pembeni yake tuliweka gogo kama mke wake.
Nakumbuka ilikuwa usiku wa manane tuliweza kufika katika kaya moja ambayo walikuwa wafugaji wa mifugo, tulichokifanya kabla hatujaenda zizini tulizizungukia nyumba zote na kumwaga dawa juu ya paa.
Malengo ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuwafanya wasisikie chochote kinachoendelea nje (walale fofo).
Tulifikia eneo la zizi na kuanza kutoa miti iliyotumika kufunga mlango kwa umakini mkubwa ikiwa mimi ndio kiongozi wa mambo.
 Tuliweza kuingia zizini na kuchagua dume la kondoo lililonona, niliichinja humo humo ndani ya zizi na damu iliweza kutapakaa ndani ya zizi, baadae tukanyanyua na kupeleka nyumbani. 
Kabla hatujaondoka tuliweza kuweka alama za nyayo ya fisi , ili kusudi wakiamka waamini kuwa aliwavamia fisi.
Baada ya siku tatu, ya nne mama aliweza kutupa majina ya wanafunzi wanaostahili kupelekwa GAMBOSHI kwa ajili ya kuliwa kwenye sherehe ya dunia iliyotarajiwa kufanyika nchini Nigeria.
Mama alitupa majina ya watu saba, watatu walikuwa wanafunzi, mmoja mwalimu na watatu ni vijana wa mitaani.
Mama alidai kuwa hao wote aliowachagua walikuwa wakiwaonea sana watoto wake bora wakaliwe nyama.
Tukiwa watatu mimi, Sheila na bibi tuliweza kufika shuleni.
 Tulianza kumimina dawa kila nje ya milango ya madarasa na ya walimu.
Kipindi hicho hakuna aliyetuona.
Tukiwa tunamimina dawa nilishangaa kumuona bibi akianguka chini na kupiga kelele kama mtoto mdogo.
 Hapo ndipo nilishuhudia wanafunzi wakipiga kelele na kushangilia huku wanatoka madarasani na kuelekea ofisini na wengine wakimzingira bibi.
Baada ya muda mfupi wanakijiji walijaa shuleni na kumuamuru bibi avue nguo, kweli alivua nguo zote na alibakia kama alivyozaliwa...
Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com

Share:

Saturday, October 25, 2014

Thursday, October 23, 2014

Maajabu!! MZEE AZIKWA AKIWA AMEKAA NDANI YA JENEZA

Jeneza la Kiti
Kuna taarifa ambazo kama ukibahatika zikakufikia, zinaweza kukuacha kinywa wazi ama kukushtua kwa namna fulani.

Habari kutoka 254 Kenya ni ile inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.
Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamesema ni utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea kuwalinda watoto wake pamoja na jamii yake.
Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa akisema, “Mazishi kama hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati wa mfalme Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala hatoridhika… Ataonekana akitembea huku juu….”
Baada ya mazishi hayo ya kipekee, walichukuliwa ng’ombe dume wawili na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya kufukuza mapepo wachafu, huku wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa mazishi ya hadhi.
Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia wanoishi katika Kaunti ya Kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao unaowavutia watalii eneo hilo la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo.
Share:

Sunday, October 19, 2014

KUTANA NA KISIMA CHA MAAJABU,UKINYWA MAJI YAKE UNAFANIKIWA KIMAISHA,KIPO DODOMA,ANGALIA PICHA HAPA

Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM] .Unaambiwa ukinywa maji ya kisima hicho unafanikiwa katika maisha yako
Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.

Mkuu wa kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akinywa maji yaliyochotwa kisima cha Bwibwi kilichopo Kijiji cha Iyubu Manispaa ya Dodoma, Kisima hicho kinachoaminika ni cha maajabu na mtu anayetumia maji yake hupata Mafanikio ya kiafya na kimaisha
Share:

Saturday, October 18, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" LEO SEHEMU YA 4 HII HAPA


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya NNE ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 4

Mtunzi; Timotheo Mathias
Simu yake-0765676242(WhatsApp)

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa

Ilipoishia...........................
Nilibebwa na kupelekwa kusikojulikana maana nilikuwa sioni, macho yangu yaliziba na kuwa kipofu. 

Nilipelekwa sehemu ambayo nilihisi kama nimeingizwa kwenye handaki.

Nilipofikishwa hapo ghafla nilianza kuhisi joto na mwili mzima kuniwasha.

Mara nikaanza kusikia harufu ya damu ya binadamu na kusikika sauti ikisema omba sara ya mwisho.

 Kabla sauti haijamalizika nilisikia kishindo kikitua mbele yangu, baada ya muda kidogo nilipokea kofi takatifu la usoni ambalo lilinipeleka mpaka chini ambapo niliweza kuangukia kwenye moto.
Endelea....................


Baada ya kupokea kofi takatifu nilipoteza fahamu sikuweza tena kujitambua kutokana na maumivu ya moto niliyoyapata.
Nilikuja kuzinduka nipo chini ya mti nikiwa na Sheila akiwa ananihudumia huku mwili wangu ukiwa umepakwa dawa za majani mabichi yaliyopondwa hasa sehemu niliyoungua moto.

Nikiwa najisikia maumivu nilimtazama Sheila kwa huruma na kunyanyua mkono wangu wa kuume, naye Sheila aliupokea.


Nikamuuliza "Nimefikaje hapa? Na wewe umenionaje?" Aliuchukua mkono wangu taratibu!!!!!! Huku machozi yakimtiririka na kisha alinisogelea na kunikumbatia huku akitabasamu na kusema..."Timothy amini usiamini nimekuhudumia siku tano bila ya wewe kujitambua siamini leo umezinduka!!" .Sheila alipomaliza kunieleza alinikumbatia tena kwa furaha, nikamuuliza hapa nimefikaje??Sheila alinyamaza kwa muda kisha akasema


"Ni stori ndefu sana, siku moja nilikuwa nimekaa na misukule wenzangu babu mmoja alinitokea na kuniuliza Timothy unamfahamu??? 


Nikamjibu ndiyo namfahamu akaniambia leo ni siku ya pili amepoteza fahamu tena alienda kutupwa baada ya kugundulika kuwa alikuwa amekufa, nilishtuka na kumuuliza yupo wapi?????


Babu alinichukua na kunileta mpaka hapa ulipo na kuanza kukata kata majani na kuyaloweka mwenye maji na mengine nikakupaka mwilini mwako".Wakati Sheila anaendelea kunisimulia ghafla  nyoka mkubwa alikuja sehemu tulipokuwa tumekaa na Sheila.


Kadri nyoka huyo alivyokuwa anatusogelea Sheila naye alizidi kuondoka na kuniacha peke yangu maana mimi nilikuwa bado sijapata nguvu za kutosha.Nyoka alipanua mdomo wake na kunitemea mate mwili mzima, nilipiga kelele kutokana na maumivu niliyokuwa nayapata, ghafla nilipata nguvu na kunyanyuka na kukimbia huku nikiendelea kupiga kelele. 


Ghafla mbele yangu Babu alitokea na kuanza kunicheka, nilipogeuka nyuma nyoka sikumuona tena.


 Babu nilimuuliza nyoka yupo wapi? Babu akatabasamu na kusema ina mpaka sasa hujanizoea tu????.


Babu akasema sikia kijana mpaka kufikia hapo nimetumia nguvu zangu binafsi, kwanza macho yako nimeyatengeneza kwa kutoa upofu uliokuwa umepewa na kisha kumleta Sheila aje akuhudumie.


 Babu nilimuuliza,mbona pete yangu  siioni? 


Babu akajibu pete niliichukua kwa sababu nilihofia  mkuu wa wachawi angeichukua maana nguvu alizokuja nazo sio za kawaida. Wakati naongea na Babu,Sheila alikuwa amesogea karibu yangu na  yote aliyokuwa anayasema Babu aliyasikia.Ghafla kilitokea kimbunga kilichoambatana na upepo mkali na vumbi, baada ya muda Babu alinishika mkono wa kushoto na kunivalisha pete.Baada ya muda babu alipotea na kutoweka kimiujiza.Dakika chache mkuu wa wachawi alitokea mbele yetu na kunyanyua mkono wake huku akitusonta kidole, tulijikuta tumefika kambini. 


Kama kawaida tukajichanganya na misukule wenzetu na stories zikaanza kuchukua nafasi yake na masela (misukule) ambao ni wageni bado ndimi zao hazijakatwa.Nilishangaa kumuona mkuu wa wachawi akija sehemu tuliyokuwa tumekaa na moja kwa moja mpaka sehemu nilipokuwa nimekaa akanishika mkono na kuondoka naye.


Tuliondoka na kuingia porini, mbali kidogo na kambi, tulifika sehemu kulikuwa na mti mdogo

tulisimama. 

Mkuu alisema "kijana una nyota kali sana haijawahi kutokea kwa mtu nimemuua aje apone?!! Kama ulivyofanya wewe , sasa basi nitakachokuambia naomba  ufanye".Babu alinyoosha mkono wake na shoka kali likatua mkononi mwake na kuniamuru nichukue shoka.Shoka nillilichukua nikalishikilia. Mkuu aliniambia nigeuke nyuma yangu na kuniamuru niukate mti ambao tulikuwa tumesimama nikamjibu kwa kujiamini HAKUNA TABU MKUU!!!!!!!!!!!!!!!!. 


Mti niliusogelea na kujitemea mate mkononi na kuishika shoka kisawa sawa nikainyanyua kwa nguvu zangu zote na kuliachia kwenye mti.Duh!! kabla shoka halijatua nilishaanga kuona sura ya mama wakati nilimuacha nyumbani.


Itaendelea sehemu ya 5 wiki ijayo Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com
Share:

Tafuta Habari Hapa

Subscribe You Tube Channel Yetu

 Bofya Hapa

Pakua Videozetu App

Kutana Able wa Michoro

Manju Matemba - Beni

Manju Polosho Myogela

Habari Kuu

TAZAMA HAPA VIDEO 100 ZA NGOMA ZA ASILI ...ANGALIA KAMA UTAONA KABILA LAKO

Habari za leo mpenzi msomaji wa Malunde1 blog hususani wewe mfuatiliaji wa nyimbo za asili..Leo nimeamua kukuletea  nyimbo zaidi ya 100 za ...

Classic Visual Shinyanga

Habari Gumzo Mtandaoni

Mshana Computer Solution

Habari Zilizopita

Jiunge Nasi Hapa

Translate This Blog

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde