Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Sunday, April 23, 2017

TAMISEMI YABARIKI MICHUANO YA COPA UMISSETA 2017 – COCA-COLA KUENDELEA NA UDHAMINI


Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na SerikalizaMitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa mishindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Share:

KAULI YA JERRY MURO BAADA YA TFF KUMFUNGIA HAJI MANARA KUTOJIHUSISHA NA MAMBO YA SOKA MWAKA MMOJA

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Haji Manara (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba) kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia anatakiwa kulipa faini ya Shilingi  Milioni tisa.
Share:

TFF YAIPOKONYA POINTI TATU SIMBA SC ILIYOPEWA KUTOKA KAGERA SUGAR

Hatimaye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipokonya pointi tatu Simba SC, ilizokuwa imepewa kutoka kwa Klabu ya Kagera Sugar.
Share:

Saturday, April 22, 2017

WATU SABA WAMEFARIKI WAKITAZAMA MECHI YA MANCHESTER UNITED NCHINI NIGERIAWatu saba walifariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kugongwa na nguvu za umeme wakitazama mechi kati ya Manchester United ya Uingereza na Anderlecht ya Ubelgiji nchini Nigeria.
Share:

Monday, April 10, 2017

JINSI SIMBA ILIVYOPATA USHINDI WA KIHISTORIA DHIDI YA MBAO UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA

Simba wamepata ushindi wa kihistoria dhidi ya Mbao FC mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
Share:

Saturday, April 8, 2017

KAGERA SUGAR, JKT RUVU WATOSHANA NGUVU KAITABA KWA SARE YA 0- 0

Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea tena Jumamosi na katika Uwanja wa Kaitaba tukishuhudia Timu ya Kagera Sugar ikitoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Timu ya JKT Ruvu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi kuu Vodacom msimu huu. 
Share:

Monday, March 13, 2017

HAYA HAPA MAJINA 26 YA WACHEZAJI 23 WATAKAOUNDA KIKOSI CHA TAIFA STARS

Machi 13 2017, kocha wa muda wa timu ya Taifa la Tanzania Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Taifa Stars. Mayanga ambaye amerithi nafasi hiyo kutoka kwa kocha Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya wachezaji hao leo.
Share:

Friday, March 10, 2017

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WATUMISHI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA - TFF

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru watumishi wawili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandiko  baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibum. Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Share:

Sunday, March 5, 2017

MTIBWA SUGAR WAIZUIA YANGA KUONGOZA LIGI KUU LEO


Siku moja baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa 24 wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mbeya City na kulazimishwa sare ya 2-2, leo March 5 2017 ilikuwa zamu ya watani wao wa jadi Yanga kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Share:

Tuesday, February 28, 2017

WATU WENYE VIPARA WASHEREHEKEA SIKUKUU YAO


Wenye vipara wakishiriki katika mchezo wa kuvutana na kamba Japan
***
Zaidi ya wanaume 30 wenye vipara kichwani nchini Japan wanaadhimisha siku kuu yao ya kila mwaka inayoshirikisha mchezo wa kuvuta kamba.
Share:

Saturday, February 25, 2017

JINSI MBOWE,WEMA,LOWASSA,RIDHIWANI KIKWETE,MGEJA NA NAPE WALIVYOKUTANA UWANJA WA TAIFA MECHI YA SIMBA vs YANGA


Mechi ya Simba vs Yanga leo imemalizika kwa ushindi wa Simba kupata goli 2-1 lakini pia imekutanisha baadhi ya viongozi kutoka vyama viwili vya kisiasa Tanzania ambavyo ni CHADEMA na CCM.
Share:

SIMBA YAFUTA UTEJA KWA YANGA....YAITANDIKA BAO 2-1 UWANJA WA TAIFA

Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.
Share:

Wednesday, February 22, 2017

POLISI AUA MWENZAKE KWA RISASI KISHA KUJIUA KWA KUJIPIGA RISASI KICHWANI


POLISI amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo na yeye amejiua baada kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya Manchester City na Monaco.
Share:

Sunday, February 19, 2017

MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA MCHEZAJI BONNY MWANDANJI

Maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wamejitokeza katika mazishi ya mchezaji wa zamani Geoffrey Bonny Mwandanji aliyefariki dunia juzi na kuzikwa katika makaburi ya kanisa Katoliki Makandana wilayani Rungwe.
Share:

Saturday, February 18, 2017

DC SHINYANGA AONGOZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI...SHUHUDIA HAPA NIMEKUWEKEA PICHA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Februari 18,2017 amewaongoza wakazi wa Shinyanga kufanya mazoezi katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga. 
Share:

Friday, February 17, 2017

TAARIFA KUHUSU KIFO CHA MCHEZAJI WA YANGA NA TAIFA STARS GEOFREY BONNY 'NDANJE'

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Prisons na Taifa Stars, Geofrey Bonny 'Ndanje' (37), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jijini Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya kifua kikuu,
Share:

Monday, January 30, 2017

Tanzia: GOLIKIPA WA KAGERA SUGAR DAVID BURUHANI AFARIKI DUNIA


Golikipa wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za ligi kuu amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Share:

Friday, January 20, 2017

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA INJILI KUTOKA KWA ANGEL THOMAS - MOYO WANGU

Msanii wa nyimbo za Injili Angel Thomas kutoka Mbeya ametualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa "Moyo Wangu".
Sikiliza na unaweza kudownload wimbo huu hapa chini.Hakika utabairikiwa sana
Share:

Sunday, January 15, 2017

Tanzia: MWANDISHI WA HABARI AMINA ATHUMANI AFARIKI DUNIA,ALIKUWA ZANZIBAR KURIPOTI MAPINDUZI CUPAmina Athumani enzi za uhai wake
Share:

Saturday, January 14, 2017

MNYAMA SIMBA ACHINJWA USIKU ZANZIBAR, AZAM FC BINGWA MAPINDUZI


Himid Mao
Klabu ya Azam ya jijini Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Simba SC ambayo pia ni ya jijini Dar es salaam kwa bao 1-0. 
Share:

Tafuta Habari Hapa

Subscribe YouTube Channel

 Bofya Hapa

Habari Kuu

BINTI ANAYEDAIWA KUFA PAPO HAPO KWA KUGONGWA NA GARI AONEKANA MAKABURINI AKIWA HAI

Kijana dereva wa bodaboda,ambaye pia ni mganga wa jadi, Anuary Abdallah akiwa na binti aliyedaiwa kugongwa na gari kisha kufariki dunia...

Video:Juma Machupi - Mwajuma

Video: Itendele Mchenya - Harusi ya Veronica

Classic Visual Shinyanga

Habari Zilizosomwa Sana Mwezi Huu

Mshana Computer Solution

Habari Zilizopita

Jiunge Nasi Hapa

Translate This Blog

Bhudagala - Bhasobhi

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde