Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAFISA HABARI WA SERIKALI LINDENI SIRI ZA SERIKALI- MSIGWA



Katibu Mkuu wa Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo Bw. Gerson Msigwa amesisitiza umuhimu wa Maafisa habari, mawasiliano, itifaki na uhusiano serikalini kulinda na kutunza siri za serikali, akisema usiri katika mawasiliano si kisingizio cha Maafisa habari wa serikali kushindwa kuwajibika katika nafasi zao kwa kutoa taarifa kwa wananchi na vyombo vya habari Nchini.

Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa serikali amebainisha hayo leo Alhamisi Mei 07, 2026, wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 21 cha Maafisa habari, mawasiliano, itifaki na uhusiano serikalini, kinachofanyika Mkoani Njombe, kusini Magharibi mwa Tanzania.

"Naomba nisisitize mambo machache, sisi ni maafisa habari, tumeanza kuona dalili za kuvuja kwa siri za serikali, na hii sio excuse ya wewe kutotoa taarifa. Siri za serikali zina utaratibu wake, kama ni barua huwa ina utaratibu, inagongwa mhuri wa siri. Tumeanza kuona nyaraka za siri zinavuja, naomba Maafisa habari kuwa wavujishaji tusiwe sisi kwasababu kwa bahati nzuri uwekezaji uliofanywa na serikali katika usalama wa mitandao, ukifanya hivyo tutajua. Msifanye hivyo, ninyi pelekeni ujumbe huu kwa watumishi wote wa serikali." Amesema Gerson Msigwa.

Kulingana na Msemaji Mkuu huyo wa serikali ya Tanzania amesema ikiwa utavujisha taarifa hizo za serikali, adhabu yake ni kufutwa kazi pamoja na kushtakiwa kwa kezi ya jinai kulinhana na sheria za nchi, akionya Maafisa habari kuwa waangalifu kwani maendeleo makubwa ya sasa katika maendeleo ya teknolojia yamerahisha ufahamu katika kumjua yule anayevujisha taarifa za serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com