Showing posts with label shinyanga. Show all posts
Showing posts with label shinyanga. Show all posts

Thursday, April 20, 2017

TAKUKURU SHINYANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUMISHI WA KANISA LA AICT KWA KUTAFUNA MILIONI 63.4


Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa  Shinyanga Gasto Mkono akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Aprili 20,2017
Share:

Sunday, April 16, 2017

Picha 45:TAMASHA LA KUIMBA NA KUABUDU VIJANA KANISA LA TAG SHIYANGA UWANJA WA SHYCOM SIKUKUU YA PASAKAKanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Shinyanga limeadhimishisha sikukuu ya pasaka kwa kufanya tamasha la kuimba na kuabudu katika uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga.
Share:

MADIWANI KAHAMA WATAKA SEKONDARI ILIYOTUMIA MIAKA 11 KUJENGWA IKAMILIKE

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Abel Shija
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,wameamuru kukamilishwa mara moja kwa ujenzi uliotumia miaka 11 katika Shule ya Sekondari Kitwana,iliyoko Kata ya Busoka,ili kunusuru wanafunzi
kutembea umbali wa kilometa 15,kufuata masomo.
Share:

Saturday, April 15, 2017

AFARIKI KWA KUGONGWA KIBERENGE RELINI AKIENDA KWENYE MKESHA WA PASAKA SHINYANGA

NB- Pichani ni mfano wa kiberenge
Habari tulizozipata usiku huu wa Jumamosi Aprili 15,2017 ni kwamba mwanamke ambaye jina lake halijafahamika mara moja amefariki dunia kwa kugongwa na kiberenge katika reli eneo la Didia wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Share:

TAZAMA HAPA NGOMA LIVE YA KISUKUMA MAARUFU "BENI" YA MANJU MATEMBA IGOMWASHU (Video)Karibu ndugu msomaji wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga hususani wewe mpenzi wa nyimbo za asili ambazo mara nyingi tunakuletea mwisho wa wiki..Leo nimekuletea Ngoma ya Kisukuma maarufu kwa jina la Beni kutoka kwa Manju anayejulikana kwa jina la Matemba Igomwashu.Hii ni ngoma iliyochezwa live kutoka uwanjani.

Hii ngoma imechezwa mwaka 2014 katika kijiji cha Itunduru wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Share:

Thursday, April 13, 2017

Audio & Picha - JESHI LA POLISI SHINYANGA LILIVYOJIPANGA KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA PASAKA


Katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka,Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu hivyo limetaka wananchi nao kujipanga kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani.
Share:

Wednesday, April 12, 2017

MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SHINYANGA


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
***
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nyanzobe Maganga (50) mkazi wa Kitongoji cha Nzanza kijiji cha Puni kata ya Puni wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga amefariki dunia kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.

Share:

Tuesday, April 11, 2017

VYUMBA MAALUM KWA WATOTO WA KIKE SHULENI NI UKOMBOZI WA MSICHANA

“ASILIMIA 10 ya fedha za huduma ya kwanza kwa shule haitoshi kuhudumia wanafunzi wote kwani shule zetu zina wanafunzi wengi, lakini tunaendelea kuangalia namna ya kuwasaidia watoto hawa ili waweze kuhudhuria masomo yao,”anasema Kahundi.
Share:

Sunday, April 9, 2017

New Video: EGAM DROPPER - MISHENI

Ninayo hapa video mpya ya msanii Egam Dropper kutoka Shinyanga inaitwa Misheni imetengenezwa na Q ze Don

Share:

Friday, April 7, 2017

Picha: WANAUME SHINYANGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUTAHIRIWA,47,500 WAPATA TOHARA BUREHuduma za tohara kwa wanaume zimeshamiri mkoani Shinyanga ambapo zaidi ya wanaume 47,500 wamenufaika na huduma hiyo katika kipindi cha Mwezi Oktoba 2016 hadi Machi 2017 kupitia kampeni ya Tohara Kinga ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kujikinga na maambukizi ya VVU. 

Share:

Picha 26: VIONGOZI WILAYA YA MEATU,KISHAPU,IRAMBA NA IGUNGA WAFANYA KIKAO KUNUSURU ZIWA KITANGIRI


Ijumaa Aprili 7,2017 viongozi wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Iramba- Singida,Igunga-Tabora na Kishapu- Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kunusuru ziwa Kitangiri ambalo lipo hatarini kupotea kutoka na shughuli za kibinadamu zinazofanyika kwenye vyanzo vya ziwa na ndani ya ziwa hilo ikiwemo kilimo na ufugaji.
Share:

Wednesday, April 5, 2017

SERIKALI YATAIFISHA KIWANDA CHA NYAMA TRIPLE 'S' SHINYANGA

Miezi mitatu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuuagiza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji mwingine,hatimaye leo Jumatano Aprili 5,2017,serikali mkoani Shinyanga imekitaifisha kiwanda hicho.
Share:

Monday, April 3, 2017

HALOTEL YAZINDUA HUDUMA YA WANANCHI KUPIGA SIMU BURE KWA JESHI LA POLISI KUFICHUA UHALIFU SHINYANGA


Kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Muliro Jumanne Muliro akiwa ameshikilia bango la uzinduzi wa huduma ya wananchi kupiga simu bure kwa  jeshi la polisi kufichua vitendo vya uhalifu katika jamii.Wa kwanza kulia ni Mkuu Wa  idara ya utawala Halotel mkoa wa Shinyanga Throng Khoa na mkuu wa idara ya Ufundi Halotel mkoa wa Shinyanga Bw.Thao.
Share:

KAULI YA ASKOFU NKOLA NA WACHUNGAJI BAADA YA KUFUKUZWA KAZI KANISA LA AICT

Aliyekuwa askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola akizungumza na Malunde1 blog kanisani baada ya askofu mkuu wa kanisa hilo kutangaza kuwachukulia hatua viongozi watano wa kanisa hilo akiwemo askofu Nkola-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Share:

News Alert!! VIGOGO WATANO WA KANISA LA AICT WATUMBULIWA SHINYANGA,YUMO ASKOFU NKOLA NA KATIBU MKUU WA KANISA JAKOBO MAPAMBANOAskofu mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi akitangaza uamuzi wa kuwachukulia hatua viongozi watano wa kanisa hilo.
*******

Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) limemstaafisha askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola na kumtaka kujiuzulu nafasi ya uaskofu askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza John Bunango kwa kushindwa kusimamia vizuri fedha za kanisa kwa ajili ya kuendesha shule ya sekondari Bishop Nkola iliyopo mjini Shinyanga.
Share:

Sunday, April 2, 2017

Picha : ADHIMISHO LA MISA YA JUMAPILI KANISA KUU LA MAMA MWENYE HURUMA NGOKOLO- SHINYANGA,TAS YATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO


Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS) kimeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino kwenye mikusanyiko ya watu ambapo leo Jumapili Aprili 2,2017 kimetoa elimu hiyo katika kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.
Share:

Audio: ASKOFU MKUU KANISA LA AICT SILAS KEZAKUBI AKIWATUMBUA MAASKOFU NA WACHUNGAJI WATATU

Askofu mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) limechukua uamuzi mgumu leo Jumapili Aprili 2,2017 ambapo askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola amestaafishwa leo huku askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza John Bunangwa akitakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia vizuri fedha za mkopo kwa ajili ya shule ya kanisa hilo.


Kanisa hilo pia limevua uchungaji wachungaji watatu wa kanisa hilo ambao ni Emmanuel Isaya,Dkt Meshack Kulwa na Jakobo Mapambano aliyekuwa katibu mkuu wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga.

Msikilize hapa Askofu mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi akitangaza uamuzi wa baraza la utendaji sinodi kuu kanisa la AICT leo katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

SIKILIZA HAPA CHINI
Share:

Saturday, April 1, 2017

Picha 31: MKUTANO MKUBWA KWENYE SHULE ILIYOKUMBWA NA MAPEPO SHINYANGA ...VIONGOZI WA DINI WASHUSHA UPAKOMachi 29,2017 mtandao huu wa Malunde1 blog uliripoti kuhusu Shule ya sekondari Imesela kuvamiwa na mapepo na kuwafanya wanafunzi kuanguka na kutamka maneno yasiyoeleweka.
Share:

Thursday, March 30, 2017

SHULE ZATAKA PEDI KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIKE SHINYANGA,DC AOMBA MSAMAHA WA KODI


Pamoja na jitihada zinazofanyika kuhakikisha kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi lakini bado changamoto kubwa ni upatikanaji wa vitambaa wakati wa hedhi "pedi"kwa watoto wa kike hasa kwa watoto wasio na uwezo.
Share:

Wednesday, March 29, 2017

Ushirikina! MAPEPO YAVAMIA WANAFUNZI SHULE YA IMESELA SHINYANGA VIJIJINI,SHUHUDIA HAPA YAKIWATESA MBELE YA MKUU WA WILAYA

Ushirikina!! Ndivyo unavyoweza kusema…Wanafunzi wa shule ya sekondari Imesela iliyopo kata ya Imesela wilaya ya Shinyanga(Shinyanga vijijini) mkoa wa Shinyanga wamekumbwa na mapepo yanayowafanya waanguke na kupiga kelele wakitamka maneno yasiyoeleweka huku wakiwataja baadhi ya watu wanaofanya ushirikina huo.
Share:

Tafuta Habari Hapa

Subscribe YouTube Channel

 Bofya Hapa

Habari Kuu

BINTI ANAYEDAIWA KUFA PAPO HAPO KWA KUGONGWA NA GARI AONEKANA MAKABURINI AKIWA HAI

Kijana dereva wa bodaboda,ambaye pia ni mganga wa jadi, Anuary Abdallah akiwa na binti aliyedaiwa kugongwa na gari kisha kufariki dunia...

Video:Juma Machupi - Mwajuma

Video: Itendele Mchenya - Harusi ya Veronica

Classic Visual Shinyanga

Habari Zilizosomwa Sana Mwezi Huu

Mshana Computer Solution

Habari Zilizopita

Jiunge Nasi Hapa

Translate This Blog

Bhudagala - Bhasobhi

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde