Monday, April 24, 2017

UMEIPATA HII YA KICHWA CHA BINADAMU ALIYE HAI KUPANDIKIZWA KWA MTU ALIYEKUFA?...SOMA HAPA

December 2017 inatarajiwa kuwa siku ya kihistoria kwenye sekta ya afya na tiba duniani ambapo utafanyika upasuaji wa kupandikiza kichwa kwa mara ya kwanza utakaofanyika mjini London ikihusisha madaktari 150 na itachukua zaidi ya saa 34.
Share:

HII HAPA ORODHA YA WATU 100 WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI MWAKA 2017

April 2017 Jarida la Times limetoa list ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani ambapo Rais wa Marekani Donald Trump ,Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Urusi Vladmir Putin wametajwa kama Marais wenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2017.
Share:

Utafiti: USAFI WA KINYWA NI KINGA YA UGONJWA WA INI

Imeelezwa kuwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ini wanaweza kuepuka kifo cha mapema kutokana na ugonjwa huo kwa kusafisha kinywa vizuri hasa kusugua meno na fizi.
Share:

ORODHA YA NCHI 20 ZINAZOTAJWA KUONGOZA KWA UBAGUZI DUNIANI

Ubaguzi wa rangi ni moja kati ya matatizo yanayosumbua dunia kwa muda mrefu na limekuwa chanzo cha migogoro katika nchi nyingi duniani kote ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Washington Post nchi nyingi kutoka Asia zimetajwa kuongoza kwa ubaguzi.
Share:

SERIKALI YATOA TAMKO WAANDISHI WA HABARI KUSHAMBULIWA VURUGU ZA MKUTANO WA CUF

Serikali imepokea kwa masikitiko taarifa za kushambuliwa na kujeruhiwa baadhi ya waandishi wa habari katika mvutano uliotokea juzi jijini Dar es Salaam kati ya wafuasi wa pande mbili zinazokinzana za Chama cha Wananchi (CUF). Tumechukua muda kidogo kulifuatilia suala hili na kubaini licha ya baadhi yao kujeruhiwa na kuripoti polisi, wapo waandishi ambao vifaa vyao vya kazi pia vililengwa katika shambulizi hilo.
Share:

WABUNGE WA UPINZANI WAITUPIA LAWAMA SERIKALI VURUGU MKUTANO WA CUF


Siku moja baada ya kutokea kwa vurugu kubwa katika mkutano wa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa kuvamiwa na genge la watu waliokuwa na silaha za moto, wabunge wa upinzani wameibuka na kuitupia lawama Serikali.
Share:

UTEUZI WA JOKATE MWEGELO CCM WAZUA GUMZO UVCCM

Uteuzi  wa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, unaonekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo.
Share:

ASKOFU GWAJIMA AKUNWA NA RAIS MAGUFULI..SASA KUNUNUA TRENI

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).
Share:

MCHUNGAJI MBARONI KWA KUFICHA WAHAMIAJI HARAMU


MCHUNGAJI wa Kanisa la Ukombozi Pentecoste lililopo eneo la Sakina jijini hapa, amekamatwa na maofisa wa Uhamiaji baada ya kubainika kuwaficha wahamiaji haramu kutoka Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 24, 2017 - NDANI NA NJE YA TANZANIAShare:

Sunday, April 23, 2017

NGORONGORO KITOVU CHA UTALII KINACHOWAVUTIA WATU MASHUHURI DUNIANI

Na Jumia Travel Tanzania
Inaonekana mwaka 2017 umeanza vizuri katika sekta ya utalii nchini Tanzania kutokana na watu kadhaa mashuhuri kuzuru vivutio vyake. Sehemu ambazo zimeonekana kuwavutia watu wengi zaidi ni hifadhi ya mbuga ya Serengeti na bonde la Ngorongoro.
Share:

TAMISEMI YABARIKI MICHUANO YA COPA UMISSETA 2017 – COCA-COLA KUENDELEA NA UDHAMINI


Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na SerikalizaMitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa mishindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Share:

Tafuta Habari Hapa

Subscribe YouTube Channel

 Bofya Hapa

Habari Kuu

BINTI ANAYEDAIWA KUFA PAPO HAPO KWA KUGONGWA NA GARI AONEKANA MAKABURINI AKIWA HAI

Kijana dereva wa bodaboda,ambaye pia ni mganga wa jadi, Anuary Abdallah akiwa na binti aliyedaiwa kugongwa na gari kisha kufariki dunia...

Video:Juma Machupi - Mwajuma

Video: Itendele Mchenya - Harusi ya Veronica

Classic Visual Shinyanga

Habari Zilizosomwa Sana Mwezi Huu

Mshana Computer Solution

Habari Zilizopita

Jiunge Nasi Hapa

Translate This Blog

Bhudagala - Bhasobhi

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde