Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MADARASA 1,360, MABWENI 17 NA NYUMBA 33 ZA WALIMU KUJENGWA NCHINI



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepanga kujenga madarasa 1,360 ili kuimarisha utekelezaji wa sera ya elimu ya miaka 10 ya lazima pamoja na kuongeza miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi na sekondari nchini.

Hayo yameelezwa leo Mei 7,2026 bungeni na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mazingira ya elimu na kuongeza upatikanaji wa huduma bora kwa wanafunzi katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Serikali itajenga mabweni 17 katika shule za sekondari 17 pamoja na nyumba 33 za walimu kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya walimu, hasa katika maeneo yenye changamoto za miundombinu.

Vilevile, vituo 50 vya walimu vitajengwa katika Halmashauri za Wilaya ili kuongeza motisha kwa walimu na kusaidia utoaji bora wa huduma za elimu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com