Na mwandishi wetu, Dodoma
Leo Februari 12, 2026 Benki ya CRDB kupitia CRDB foundation imetangaza kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kumsaidia kijana kimaendeleo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa program ya Go green iMbeju jijini Dodoma, Mkurugenzi wa CRDB Foundation Tully Esther Mwambapa amesema taasisi hiyo imeanzishwa mahsusi kusaidia jamii.
Amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha vijana wanapata ufadhili na fursa za kukuza unuzi , biashara na maendeleo yao binafsi.
Mwambapa amesisitiza kuwa CRDB Foundation itakuwa kielelezo cha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa kifedha, kwa kutoa msaada wa kifedha na maarifa kwa vijana wenye ndoto za kimaendeleo.
“Tunaamini kuwa uwekezaji kwenye vijana ni uwekezaji wa taifa,” amesema.
Awali akizindua program hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prf. Kitila Mkumbo amesema Serikali itaendelea kubaini na kufuta vikwazo vinavyowakabili vijana, ikiwemo kufuta ada za shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Waziri Mkumbo amewatahadharisha vijana hususan wenye ujuzi maalum, kutumia fursa zinazotolewa na Serikali na wadau wa kifedha kupata fedha, kukuza ujuzi, kuendeleza biashara zao na kuboresha maisha yao.
Aidha, asema Serikali itaendelea kuhimiza ushirikiano kati ya taasisi za kifedha na sekta binafsi kuhakikisha kila kijana anapata nafasi ya kufanikisha malengo yake, huku akiwataka vijana kuendeleza maadili ya bidii, uvumbuzi na ustadi wa kitaalamu.





Social Plugin