POLISI WAVAMIA OFISI ZA CHADEMA MOROGORO NA KUKAMATA VIONGOZI
Friday, September 19, 2014
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa polisi mkoani Morogoro wamevamia ofisi za Chadema wilaya na kukamata viongozi waandamizi watano wa chama hicho waliokuwa wakijiandaa kuongoza maandamano ya kupinga bunge maalum la katiba. Habari zinasema kuwa wafuasi wengi wa Chadema wamepewa vipigo na polisi hao. Inaelezwa kuwa baadhi ya nyaraka za chama hicho zimepotea Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonald Paul amesema maandamano hayo siyo halali na tayari watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin