Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UHUSIANO WA TANZANIA NA URUSI: MARAFIKI WA KWELI NA WASHIRIKA WA MAENDELEO

Tanzania na Urusi zina uhusiano wa kihistoria wenye hekima, heshima na ushirikiano wa pande mbili unaoheshimiana. 

Tofauti na nchi za Magharibi ambazo zilitumia ukoloni, unyonyaji na utumwa kuwatawala Waafrika kwa karne nyingi, Urusi haijawahi kuwa na koloni. Badala yake, imekuwa mshirika wa dhati katika mapambano yetu ya uhuru na maendeleo.

Tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Umoja wa Kisovyeti uliunga mkono kwa dhati harakati za uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. Walitoa misaada ya kielimu, kijeshi na kiuchumi kwa harakati za ukombozi barani Afrika. Maelfu ya vijana wa Tanzania walisoma katika vyuo vya Urusi na kurudi nyumbani na elimu bora.

Wakati wa Vita vya Kagera (1978-1979), Urusi iliunga mkono Tanzania kwa kusimama upande wa haki na kupunguza msaada kwa dikteta Idi Amin aliyevamia nchi yetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara rasmi ya kihistoria nchini Urusi kuanzia leo Juni 3, 2026. 

Hii ni ziara ya pili ya Rais wa Tanzania nchini Urusi katika historia ya nchi yetu. Ziara ya kwanza ilifanyika mwaka 1969 wakati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipaalikwa rasmi na viongozi wa Umoja wa Kisovyeti. Baada ya miaka 57, Rais Samia anafuata nyayo za Baba wa Taifa katika kuimarisha uhusiano huu muhimu.

Ziara hii inatarajiwa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara, nishati, madini, elimu, sayansi na teknolojia. Rais Samia anakutana na Rais Vladimir Putin Kremlin na kushiriki katika St. Petersburg International Economic Forum.

Kwa Watanzania, Hii ni fursa ya kutambua na kuthamini marafiki wetu wa kweli. Urusi inaheshimu uhuru wetu na inataka ushirikiano wa pande mbili bila masharti ya kisiasa. Tuunge mkono ziara hii ili ilete matunda halisi kwa maendeleo ya Tanzania yetu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com