Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA UJENZI YAOMBA SH. TRILIONI 2.5 KWA BAJETI YA 2026/2027



Na Dotto Kwilasa,DODOMA

Wizara ya Ujenzi imeiomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi trilioni 2.5 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu nchini.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega alisema fedha hizo zitaelekezwa katika vipaumbele sita vikuu vinavyolenga kuimarisha sekta ya usafiri na uchumi wa taifa.

Alisema miongoni mwa maeneo yatakayopatiwa kipaumbele ni ujenzi na ukarabati wa barabara kuu, barabara za mikoa, madaraja pamoja na miundombinu ya usafiri inayounganisha maeneo ya uzalishaji na masoko.

Ulega alisema Serikali inaendelea kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili kuboresha huduma za usafirishaji, kupunguza gharama za usafiri na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi nchini.

Aidha, alisema katika kipindi cha miezi 10 kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026, Serikali kupitia wakala wa barabara imefanikiwa kujenga kilometa 243.13 za barabara za lami huku miradi mingine ikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini.


Kwa mujibu wa Waziri huyo, bajeti hiyo pia itasaidia kuendelea na miradi ya kuunganisha mikoa na wilaya kwa barabara za kiwango cha lami sambamba na kuimarisha miundombinu ya mijini na vijijini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com