Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe.Denis Masanja wa pili kutoka kushoto akiwa katika mnada wa kwanza wa ufuta ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tunduru huku bei ya juu ya ufuta ufuta huo ikiwa shilingi 2520 na bei ya chini ikiwa shilingi 2410
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mheshimiwa Denis Masanja alieketi mkono wa kulia akiwa pamoja na Mwenyekiti wa TAMCU LTD Mussa Manjaule wakiangalia kwa pamoja na viongozi wa chama cha Ushirika Tunduru TAMCU bei ya juu ya ufuta iliyofikia kiasi cha shilingi 2520
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mheshimiwa Denis Masanja alieketi mkono wa kulia akiwa pamoja na Mwenyekiti wa TAMCU LTD Mussa Manjaule wakiangalia kwa pamoja na viongozi wa chama cha Ushirika Tunduru TAMCU bei ya juu ya ufuta iliyofikia kiasi cha shilingi 2520
Wakulima wa zao la ufuta waliojitokeza katika mnada huo leo Mei 21 2026 ukumbi wa Mkuu wa wilaya ya Tunduru
Na Regina Ndumbaro Tunduru-Ruvuma
Wakulima wa zao la ufuta Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameanza msimu wa mauzo wa 2026/2027 kwa matumaini makubwa baada ya mnada wa kwanza ulioendeshwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha TAMCU Limited kufanikisha mauzo ya zaidi ya kilo 900,000 za ufuta kwa bei yenye ushindani mkubwa.
Mnada huo umefanyika leo Mei 21, 2026 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Denis Masanja umeonyesha mwitikio mkubwa wa wanunuzi na kuongeza matarajio ya wakulima kupata mapato bora msimu huu.
Katika mnada huo, bei ya juu ya ufuta imefikia Shilingi 2,520 kwa kilo huku bei ya chini ikiwa Shilingi 2,410 kwa kilo moja, hali iliyotajwa kuwa ni chachu ya kuimarisha uchumi wa wakulima wa zao hilo katika wilaya hiyo.
Viongozi wa ushirika na wadau wa kilimo wameeleza kuwa ushindani wa wanunuzi katika mnada huo umechangia kupanda kwa bei na kutoa fursa nzuri kwa wakulima kuuza mazao yao kwa faida zaidi.
Aidha, TAMCU Limited imewahimiza wakulima kuendelea kuzalisha ufuta wenye ubora unaokidhi viwango vya soko ili kuongeza thamani ya zao hilo katika minada ijayo.




Social Plugin