Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, amesisitiza umuhimu wa waumini wa Kanisa hilo na Watanzania kwa ujumla kuishi katika hali ya kupokea na kutoa msamaha kama ambavyo sala kuu ya "Baba yetu uliye mbinguni" inavyowataka Wakristo kusamehe ili nao waweze kusamehewa na Mwenyenzi Mungu.
"Kazi ambayo tunayo mimi na wewe ni kuihamasisha jamii na kuikumbusha kwamba ukristo unahitaji kuishi katika hali ya kupokea msamaha ambayo Yesu mwenyewe ametuombea lakini sisi pia tutoe kwa wengine kwamaana hata katika sala kuu ya Baba yetu uliye mbinguni, tunasema Baba utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyowasamehe wanavyotukosea." Amesema Dkt. Malasusa.
Dkt. Malasusa ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na Chombo kimoja cha habari Jijini Dar Es Salaam, akisema ni muhimu kuuishi msahama katika maisha ya kila siku kama sehemu ya kutekeleza mapenzi ya Mungu, akisisitiza kila mmoja kuwajibika katika kuhamasisha msamaha kama jambo muhimu kwa anayesamehe na anayesamehewa.
Askofu Malasusa amesema kwa wakristo ni muhimu zaidi kusamehe kabla ya kwenda kwenye ibada, akisema yapo maandiko mengi katika Biblia yenye kufundisha kuhusu msamaha na kusema msamaha ni zaidi ya ibada na sikukuu nyingine ambazo wakristo wamekuwa wakisherehekea na kuadhimisha.

Social Plugin