Serikali imewaomba Viongozi wa Dini kuungana katika Kupigana Vita ya Mmomonyoko wa Maadili huku ikiweka wazi wajibu wa familia kutotekelezwa ipasavyo hali inayopelekea kuwepo kwa madhara ya mmomonyoko wa maadili huku makundi ya vijana yakijihusisha na dawa za kulevya,uporaji,ubakaji,utapeli na maasi hali itakayopelekea kuona ni halali kula jasho la mtu au kufanya mauaji ili kupata mali.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi wakati wa Kikao Kazi na Viongozi wa Dini ambapo agenda za Mmomonyoko wa Maadili,Amani na Utulivu,Matumizi sahihi ya Mitandao ya Kijamii zilitawala kikao hicho lengo ikiwa kulinda tunu ya amani iloyopo nchini.
“Hakuna bomu baya kuliko silaha za kivita kama mmomonyoko wa maadili,bomu hili linaathiri kila kukicha,nawaomba sana viongozi wa dini mtusaidie sana kupigana vita ya mmomonyoko wa maadili,familia hazitekelezi wajibu wake siku hizi kwa kiwango kikubwa hasa kwetu sisi vijana,nafurahia kuona wazee wetu mmetufikisha mpaka hapa leo Taifa limekua na amani na salama ni kwasababu ya maadili mliyokuwa nayo,vijana wenye maadili mazuri wapo hao sio tatizo kwasababu wanabeba ile hofu ya Mungu.
Lakini tukiacha mmomonyoko wa maadili uendelee kushamiri katika jamii tafsiri yake hatutokuwa salama kwasabu baadhi ya vijana ambao hatutokua na mafunzo ya kiimani tutajiingiza kwenye dawa za kulevya,wizi,uporaji,ubakaji,utapeli na maasi na kuona ni halali kula jasho la mtu kwa kudhulumu kwa sababu ya mmonyoko wa maadili,tunapenda mali kuliko watu.”Amesema Katambi



Social Plugin