Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASKOFU CHILONGANI AIOMBA SERIKALI KUSHUGHULIKIA RUSHWA, UKIRITIMBA NA KERO ZA WANANCHI



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika,Dkt Dickson Cholongani ameiomba Serikali kuongeza jitihada za kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo rushwa, ukiritimba pamoja na kunyimwa haki katika baadhi ya taasisi na ofisi za umma.

Akizungumza katika mahubiri ya Pasaka yaliyofanyika katika Kanisa la Paulo wa Msalaba Jijini Dodoma, Askofu huyo amesema licha ya kuwepo kwa mafanikio kadhaa ikiwemo ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma, bado wananchi wengi wanakumbana na changamoto zinazopunguza furaha na ustawi wao.

Alisema miongoni mwa kero zinazoendelea kujitokeza ni pamoja na vitendo vya rushwa vinavyofanyika waziwazi, ambapo baadhi ya watumishi hudaiwa kuomba.

"Tunashukuru mwaka jana mishahara iliongezwa. Lakini bado kuna kero nyingi kwenye maofisi. Kero za ukiritimba, kero za kunyimwa haki, kero za rushwa. Sasa hivi 'facilitation' zinaombwa wazi wazi.

"Unamtuma mfanyakazi ashughulikie suala muhimu anakwambia Baba Askofu tukienda wanatuomba facilitation. Hawaoni aibu hata kuliomba Kanisa litoe facilitation. Tuiombe serikali itupie macho kero hizi ili Watanzania waishi kwa furaha,"alisema Dkt Chilongani

Aidha, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano nchini, akisisitiza kuwa jitihada zaidi zinahitajika ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa furaha na haki inatendeka kwa wote.

Dkt Chilongani ameitaka jamii kwa ujumla kushiriki katika kujenga taifa lenye maadili mema, huku akisisitiza kuwa Pasaka ni kipindi cha matumaini, mabadiliko na kuondoa mizigo inayowakabili wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com