Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUCHAKATA UFAULU KISHAPU, WAZEMBE "KUKIONA"


. Na Sumai Salum- Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na mwenyekiti wa kikao Cha wadau wa elimu wilayani humo Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa elimu kuhusu tathmini ya ufaulu wa mwaka 2026 kuanzia shule ya awali na msingi Hadi sekondari kidato Cha sita kilichofanyika Machi 26,2026 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kishapu wilayani humo


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga , Mhe.Peter Masindi, ameonya vikali kushuka kwa kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 71 % mwaka 2025 hadi kufikia 61% mwaka 2026 katika shule za awali na msingi wilayani humo huku shule za sekondari zikijitahidi kufanya vizuri ambapo ufaulu wa kidato cha sita ni 100% mwaka 2026, amesisitiza uwajibikaji kwa watendaji wote wa sekta ya elimu.


Akizungumza Machi 26, 2026 katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Masindi akiwa ndiye Mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa kushuka kwa ufaulu hadi kufikia asilimia 10 ni dalili ya uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya chini hadi wilayani.


Amesema Afisa Elimu anapaswa kusimamia majukumu yake ipasavyo, akibainisha kuwa uzembe katika nafasi hiyo ni chanzo kikuu cha kushuka kwa ufaulu. “Serikali haiko tayari kuvumilia kushuka kwa ufaulu. Wale wote watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao wanapaswa kujitathmini au kupisha wengine wenye uwezo, wasimamie nafasi hizo” amesisitiza Masindi.


Katika kuboresha elimu, Masindi ameelekeza kuwa wadhibiti ubora na waratibu wa elimu wawe mstari wa mbele kufika mashuleni kufuatilia maendeleo ya wanafunzi, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga msingi imara wa elimu kuanzia ngazi ya awali hadi sekondari.


Aidha, ameagiza kuwa walimu wenye weledi na bidii wapewe nafasi za uongozi ili wasimmaie kwa nguvu suala la ufaulu kuongezeka na suala la Lishe mashuleni, ameonya kuwa yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa suala la lishe kwa wanafunzi atachukuliwa hatua kali.


Akitoa taarifa ya elimu ya awali na msingi, Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi, Boas Mafuru, amesema baadhi ya changamoto zilizosababisha kushuka kwa ufaulu ni pamoja na ukosefu wa chakula kwa baadhi ya shule, ufundishaji usio na viwango kwa baadhi ya walimu, usimamizi dhaifu kwa baadhi ya walimu wenye dhamana ya uongozi, ukosefu wa hamasa ya masuala ya elimu kwa baadhi ya wazazi na utoro wa wanafunzi.


"Mhe. Mwenyekiti Divisheni imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhamasisha kilimo cha mazao ya chakula katika shule zote 128 za awali na msingi ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni, pamoja na kuimarisha usimamizi wa ufundishaji na kufanya tathmini za mara kwa mara kwa wanafunzi". amesema Mafuru


Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya walimu, wazazi na walezi katika kupambana na utoro na kuboresha mazingira ya ujifunzaji.


Kwa upande wao, wadau wa elimu wakiwemo TCRS, CRDB Bank, NMB Bank, wazee maarufu na viongozi wa dini wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu, ikiwemo ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo huku wakiahidi kutumia majukwaa yao ya dini kuhubiri umuhimu wa elimu kwa jamii na lishe kwa watoto hasa shuleni.


Katika kikao hicho, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Fadhili Mvanga, amekabidhi vyeti vya pongezi kwa shule 10 zilizofanya vizuri, huku shule zilizofanya vibaya zikipewa vinyago kama njia ya kuhamasisha kuongeza juhudi za kuinua ufaulu.


Ikumbukwe kuwa, Wilaya ya Kishapu hali ya Ufaulu wa elimu sekondari mwaka 2025 kidato cha pili ulikuwa 86% na mwaka 2026 ni 86% na kidato cha nne ufaulu mwaka 2025 ulikuwa 84% kwa mwaka 2026 umeongezeka na kuwa 93%.Kaimu Katibu Tawala wa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fadhili Mvanga, akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa elimu kuhusu tathmini ya ufaulu wa mwaka 2026 kuanzia shule ya awali na msingi Hadi sekondari kidato Cha sita kilichofanyika Machi 26,2026 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kishapu wilayani humoMwenyekitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe, akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa elimu kuhusu tathmini ya ufaulu wa mwaka 2026 kuanzia shule ya awali na msingi Hadi sekondari kidato Cha sita kilichofanyika Machi 26,2026 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kishapu wilayani humo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga Jacobo Ngainayo, akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa elimu kuhusu tathmini ya ufaulu wa mwaka 2026 kuanzia shule ya awali na msingi Hadi sekondari kidato Cha sita kilichofanyika Machi 26,2026 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kishapu wilayani humoKaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga Boas Mafuru, akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa elimu kuhusu tathmini ya ufaulu wa mwaka 2026 kuanzia shule ya awali na msingi Hadi sekondari kidato Cha sita kilichofanyika Machi 26,2026 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kishapu wilayani humo

Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga Winfrida Mukama, akiwa kwenye kikao Cha wadau wa elimu kuhusu tathmini ya ufaulu wa mwaka 2026 kuanzia shule ya awali na msingi Hadi sekondari kidato Cha sita kilichofanyika Machi 26,2026 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kishapu wilayani humo






















































































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com