Na. OWM-KAM, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhia mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano kwa mwaka wa Fedha 2026/2027 huku ikipongeza utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/26.
Akizungumza baada ya majadiliano ya wajumbe leo Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu amesema Kamati imeridhia bajeti ya Wizara hiyo kumpongeza Waziri anayesimamia, Mhe. Deus Sangu kwa kazi nzuri ya uwasilikishaji wa taarifa kwa kamati.
“Tunakupongeza Waziri kwa utekelezaji mzuri wa kazi ikiwemo bajeti iliyopita 2025/25 pamoja na usimamizi wa miradi iliyo chini ya Wizara kama kiwanda cha chai Mponde, kiwanda cha Ngozi cha Kilimanjaro (KLICL), mradi wa jengo la kitega uchumi Mzizima , mafunzo ya uangagenzi chuo cha wananchi Kigamboni na mfumo wa e-UTATUZI ambayo tuliitembelea hivi karibuni” alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha , Kamati hiyo ya Bunge imetaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza nafasi za vijana watakaopata mafunzo ya kuongeza ujuzi kupitia uanagenzi pamoja na kusimamia kwa karibu fursa za ajira nje ya Nchi kwa kuhakikisha watanzania wanaokwenda huko wanapata malipo mazuri na mikataba yenye tija.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu aliiomba Kamati hiyo kupitisha bajeti ili serikali ikatekeleze shughuli za ukuzaji fursa za ajira, huduma kwa wananchi na miradi ya maendeleo kama ilivyoanishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Dira 2050.
Vilevile, Waziri Sangu aliwahakikishia wajumbe wa kamati hiyo kuwa Serikali itatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ili kuwezesha wananchi na wadau kunufaika na matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kadhalika, amesema utekelezaji wa mfumo wa kielektoniki wa usajili na utatuzi wa migogoro uliozinduliwa mwaka huu (e-UTATUZI) Waziri Sangu aliwajulisha wabunge kuwa Ofisi yake itaanda semina ya kuwajengea uwezo ili waweze kuwa mabalozi wa kutangaza na kueleimisha wananchi kutumia mfumo huo wa serikali kufikisha malalamikoyao na kupata ufumbuzi bila gharama za kusafiri kufuata ofisi za Tume Usuluhishi na Utatuzi (CMA).



Social Plugin