Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MISA TANZANIA WATINGA IRINGA, WAANDISHI NA WAHARIRI WASHUHUDIA VIVUTIO, WAAHIDI KUWA MABALOZI WA KWELI WA UTALII


Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Waandishi wa habari na wahariri kutoka maeneo mbalimbali nchini wametembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa kwa lengo la kuvitangaza na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia utalii wa ndani.

Ziara hiyo imefanyika sambamba na kongamano la MISA TAN Summit 2026 lililowakutanisha wadau wa habari kujadili fursa za maendeleo pamoja na nafasi ya vyombo vya habari katika kukuza sekta ya utalii.

VIVUTIO WALIVYOTEMBELEA

Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Isimila Stone Age Site, eneo lenye umuhimu mkubwa kihistoria likiwa na mabaki ya zana za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale pamoja na nguzo za mchanga zilizoundwa kwa maelfu ya miaka.

Pia wametembelea Gangilonga Rock, jiwe lenye historia ya asili ya Wahehe na sehemu nzuri ya kutazama mandhari ya mji wa Iringa; Chief Mkwawa Memorial Site, eneo la kumbukumbu ya Chifu Mkwawa lenye mchango mkubwa katika historia ya upinzani dhidi ya ukoloni.

Kivutio kingine ni Forestry and Wood Industries Training Centre (FWITC), kituo cha mafunzo kinachohusu misitu na viwanda vya mbao ambacho pia ni kivutio kwa wanaopenda uhifadhi wa mazingira.

Hali kadhalika wamefika Sao Hill Forest Plantation, moja ya mashamba makubwa ya miti barani Afrika yanayovutia kwa uzuri wa asili na mchango wake kiuchumi; pamoja na Iringa Boma, jengo la kihistoria la enzi za Wajerumani ambalo sasa linatumika kama makumbusho ya historia ya mji wa Iringa.
SERIKALI YATAJA IRINGA KITOVU CHA UTALII

Akizungumza Machi 17, 2026 wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James amesema mkoa huo ni kitovu cha utalii katika Kanda ya Kusini kutokana na wingi wa vivutio.

Amevitaja vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Ruaha National Park, Udzungwa Mountains, pamoja na maeneo ya kihistoria kama Isimila na Kalenga, na mashamba ya miti ya Sao Hill.

Kwa upande wao, washiriki wa kongamano hilo wamesema ziara hiyo imewapa uelewa mpana kuhusu rasilimali za utalii zilizopo nchini.

Wamesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kubadili mtazamo wa jamii kwa kuandaa maudhui yatakayohamasisha Watanzania kushiriki utalii wa ndani.
MISA TANZANIA: WAANDISHI WAWE MABALOZI WA UTALII

Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko amesema lengo ni kuwafanya waandishi wa habari kuwa mabalozi wa kuitangaza Tanzania.

Amesema kupitia kalamu na vyombo vya habari, wanahabari wanaweza kuhamasisha jamii kutembelea vivutio vya utalii na hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Sekta ya utalii ni moja ya nguzo kuu za uchumi wa taifa, hivyo juhudi za kuutangaza kupitia vyombo vya habari zinaweza kuongeza idadi ya watalii na kukuza uchumi katika maeneo mbalimbali nchini.

Kitendo cha MISA Tanzania kuunganisha kongamano hilo na utalii wa ndani inalenga kuwajengea wanachama wake uwezo wa kuwa mabalozi wa kweli wa kuitangaza Tanzania.


MISA TANZANIA WAFANYA UTALII WA NDANI IRINGA KUTANGAZA VIVUTIO




Na Marco Maduhu, IRINGA




Wahariri na waandishi wa habari wanaoshiriki kongamano la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA Tanzania) wamepata fursa ya kufanya utalii wa ndani mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.


Ziara hiyo imefanyika leo Machi 18, 2026 ikiwa ni sehemu ya siku ya pili ya kongamano la MISA TAN Summit 2026, ambapo washiriki walitembelea hifadhi mbalimbali kujionea vivutio vya utalii ikiwamo Makumbusho ya Chifu Mkwawa.




Akizungumza kuhusu ziara hiyo Mwenyekiti wa Misa Tanzania Edwin Soko, amesema, lengo ni kuwafanya waandishi wa habari kuwa mabalozi wa kutangaza vivutio vya utalii wa ndani, kwa kutumia kalamu na vyombo vya habari kuhamasisha Watanzania kutembelea maeneo ya vivutio hivyo.




Amesema Iringa ni miongoni mwa mikoa yenye fursa kubwa za utalii, zikiwemo hifadhi za taifa, mandhari ya kuvutia na urithi wa kihistoria, hivyo kuna umuhimu wa vyombo vya habari kusaidia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com