Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RABIA AFANYA ZIARA SHINYANGA, AAGIZA WAKALIMANI WA LUGHA ZA ALAMA KWENYE OFISI ZA UMMA

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kitaifa (SUKI) Rabia Abdallah Hamid, ameagiza Ofisi zote za umma ziwe na namba za wakalimani wa lugha za alama, kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye usikivu hafifu wanapofika kwenye ofisi hizo kupata huduma, na kuwaita haraka ili watoe usaidizi wa mawasiliano.

Ametoa agizo hilo leo Machi 27,2026 wakati akiongea na makundi mbalimbali kwenye mkutano wake mjini Shinyanga, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Amesema, kuanzia kesho anataka kuona Ofisi zote za umma zinakuwa na namba za wakalimani wa lugha za alama, ili kutoa usaidizi wa mawasiliano kwa watu wenye usikivu hafifu wanapofika kupata huduma, pamoja na kuwagharamia wenyewe na siyo watu wenye ulemavu.
“Naagiza Ofisi zote za umma ziwe na namba za wakalimani wa lugha za alama, ili mtu mwenye usikivu hafifu anapohitaji huduma apigiwe simu haraka na kufika kutoa usaidizi wa lugha na siyo mtu mwenye ulemavu atafute mkalimani wake na kumgharamikia, hilo siyo jukumu lake ni la taasisi husika,” amesema Rabia.

Aidha, amewaagiza pia watendaji wa serikali pamoja na madiwani wawe wanafanya mikutano ya mara kwa mara kwa kusikiliza kero za wananchi, wakiwamo watu wenye mahitaji maalumu, na kuzitafutia ufumbuzi, na siyo hadi kusubiri ziara za viongozi wakubwa ndipo watoe kero zao, sababu zingine zinamalizwa ngazi ya chini.


Katika hatua nyingine, amekabidhi ilani ya CCM 2025-2030 yenye maandishi ya nukta nundu, pamoja na yenye maandishi makubwa kwa ajili ya watu wenye uoni hafifu, ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya wahitaji hao.

Nao baadhi ya watu wenye ulemavu, wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa Chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga (SHIVYAWATA) Richard Mpongo, wamewasilisha kero zao mbalimbali kwa kiongozi huyo, ikiwamo ya kukosa wakalimani wa lugha za alama kwenye ofisi za umma na hivyo kushindwa kupata huduma stahiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema ujio wa kiongozi huyo ni darasa la watendaji wa serikali, kwamba wawe na tabia ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitatua, sababu nyingine zipo ndani ya uwezo wao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amesema maelekezo yote ambayo yametolewa na kiongozi huyo watayafanyia kazi kwa ustawi wa wananchi.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Katibu wa NEC, siasa na uhusiano wa kitaifa (SUKI) Rabia Abdallah Hamid akizungumza.
Katibu wa NEC, siasa na uhusiano wa kitaifa (SUKI) Rabia Abdallah Hamid akizungumza.
Katibu wa NEC, siasa na uhusiano wa kitaifa (SUKI) Rabia Abdallah Hamid akizungumza.
Katibu wa NEC, siasa na uhusiano wa kitaifa (SUKI) Rabia Abdallah Hamid akizungumza.
Katibu wa NEC, siasa na uhusiano wa kitaifa (SUKI) Rabia Abdallah Hamid akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com