Serikali imezitaka taasisi za fedha nchini kuelekeza nguvu na uwekezaji kwa wajasiriamali pamoja na wabunifu wa kidijitali waliojikita katika biashara ya nishati ili kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya taifa ya kuhakikisha asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Naibu Waziri amewasisitiza wasambazaji wa gesi ya mitungi kuongeza vituo vya usambazaji na ujazaji ili kurahisisha upatikanaji wa nishati hiyo kwa wananchi wengi zaidi, huku akiwahamasisha wabunifu na vijana walioko vyuoni kufanya tafiti na kubuni teknolojia zitakazorahisisha usambaaji wa ajenda hiyo nchi nzima.
Mradi huo uliomalizika shuleni hapo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali linalozitaka taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ili kulinda afya za binadamu na kutunza mazingira, hatua inayokwenda kuokoa gharama kubwa kwani shule hiyo yenye wanafunzi 555 imekuwa ikitumia wastani wa shilingi milioni 10.5 kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya ununuzi wa kuni pekee.
Social Plugin