Tofauti
na mabango ya kawaida ya tahadhari, mabaki ya magari yaliyoharibika huwasilisha
ujumbe kwa nguvu zaidi kwa kuonyesha athari halisi za uzembe na ukiukwaji wa
sheria za usalama barabarani kunavyohatarisha maisha ya watu.
Wataalamu
wa usalama barabarani wanasema mbinu hiyo imeanza kuzaa matunda, wakieleza kuwa
madereva wengi huzoea alama na mabango ya tahadhari, lakini hawawezi kupuuza
ushahidi wa moja kwa moja wa madhara ya ajali unaoonyeshwa wazi.
Hatua
hiyo imeonekana kubadili mtazamo wa hatari kutoka kuwa dhana ya kawaida na ya
mbali, hadi kuwa tukio linaloweza kutokea wakati wowote kwa dereva yeyote.
Je unafikiri nchini Tanzania mbinu hii inaweza kuleta matokeo chanya kwa kupunguza ajali za barabarani?

Social Plugin