Breaking : BASI LAGONGA TRENI KIGOMA MJINI....WATU ZAIDI YA 7 WAMEFARIKI


Habari tulizozipata kutoka mkoani Kigoma asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018 ni kwamba,Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi.

Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa watu waliofariki, huku idadi ya vifo ikitajwa kuweza kuongezeka, kutokana na majeruhi wengi kuwa kwenye hali mbaya.

Kamanda Otieno amesema kwa sasa jeshi la polisi lipo eneo la tukio likiendelea kuokoa miili na majeruhi wengine, na taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.



 Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527