FACEBOOK YATANGAZA KUBORESHA HABARI ZAKE

Mmiliki wa facebook Mark Zuckerbag


Kampuni ya facebook imetangaza kuwa imebadili kampuni inayoipa habari, ili kukabiliana na kile ilichotaja kama habari za uzushi na za kupotosha.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo ya facebook, Mark Zuckerberg, amesema mtandao wake sasa utakuwa ukiwauliza matumiaji wake ni vyanzo vipi vya habari wanaamini zaidi na hivyo kuwapa nafasi ya kwanza.

Waandishi wa habari wanasema kuwa kampuni hiyo ya facebook ambayo ina zaidi ya watumiaji bilioni mbili, inataka kusitisha usambazaji wa habari bandia na propaganda, baada ya mahusiano yaliyojawa na malumbano na mashirika ambayo yana misimamo mikali ya kisiasa.

Mapema mwezi huu, Mark Zuckerberg, alitangaza mabadiliko ya vyanzo vya habari ya kampuni hiyo, iliyonuiwa kuhimiza ujumbe zinazotumwa na familia na marafiki badala ya mashirika ya kibiashara na bidhaa.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527