AZAM FC YAIPIKU SIMBA...YATINGA KILELENI

Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC imeipiku Simba na kutinga kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika mchezo huo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Yahya Zayd dakika ya 70 pamoja na Paul Peter dakika ya 82.

Kwa matokeo hayo sasa Azam FC imefikisha alama 30 baada ya michezo 14 na kukaa kileleni ikiizidi Simba yenye alama 29 baada ya mechi 13.

Hata hivyo Azam FC itakaa kileleni kwa muda ikisubiri matokeo ya mechi ya kesho kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba itakayopigwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Azam FC imekuwa na rekodi nzuri kwenye michezo yake dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine ambapo haijawahi kupoteza mchezo tangu ipande ligi kuu mwaka 2017.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527