'CHUPI' MATATANI LINDI

Mfanyabiashara wa duka kata ya Chamazi, wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Mateso Chupi (39) amefikishwa mahakama ya wilaya ya Lindi, akikabiliwa na shitaka la kukutwa na vipande sita vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Tsh,67,365,000 visivyo halali. 



Chupi amefikishwa kwa Hakimu wa Mahakama ya wilaya hiyo, Mussa Ngaru, Januari 19 mwaka huu, na kusomewa shitaka linalomkabiri na mwanasheria wa serikali, Abdurahamani Mohamedi.

Mshitakiwa Chupi inadaiwa kukamatwa na vipande hivyo vya Meno,eneo la kituo cha kuuzia Mafuta mjini Liwale Septemba 27/2008,na kufanikiwa kuwatoroka askari na kwenda kuishi nchi Jirani ya Msumbiji.

Mshatakiwa amekamatwa nchini Msumbiji Januari 16 mwaka huu,na askari Polisi waliokuwa wakimsaka kwa udi na ubani kwa muda mrefu.

Akisomewa Shitaka linalomkabiri mbele ya Hakimu Ngaru, mwanasheria wa Serikali Abdurahamani Mohamedi alidai mshitakiwa alikamatwa na askari Polisi akiwa na vipande hivyo sita,Septemba 27/2008,akiwa tayari kuvisafirisha kuelekea kutafuta soko.

"Mh,Hakimu huyu mshitakiwa alikutwa eneo la kituo cha kuuzia Mafuta pale Liwale mjini,akijiandaa kwa safari,lakini kabla ya kuondoka alikamatwa na askari Polisi"Alisema Mohamedi.

Mwanasheria huyo alidai kuwa mshitakiwa ambaye hakutakiwa kujibu wala kukataa amefanya kosa chini ya kifungu cha (70) kifungu kidogo cha (1) na (2) na (3) cha Sheria na (283) na kifungu cha (57) cha Sheria ya Uhifadhi wanyama pori namba 5/2009,ikisomwa pamoja na Sheria ya hujumu uchumi,sura ya 200 marejeo ya 2002.

Hata hivyo mshitakiwa hakutakiwa kusema lolote, kwani Mahakama hiyo kisheria haina uwezo wa kusikiliza kesi za aina hiyo hadi hapo itakapopata kibari kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Mshitakiwa Mateso Chupi amepelekwa rumande ambapo kesi hiyo namba 01/2018,itafikishwa tena katika Mahakama hiyo Januari 31 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527