Breaking News!! MTOTO AUAWA KWA KUNYONGWA KISHA KUTUPIWA KWENYE KARO LA MAJI AKICHUNGA MBUZI SHINYANGA
Sunday, September 14, 2014
Habari za hivi punde zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 9 ameuawa kwa kunyongwa na mwanamme ambaye hakujulikana jina wala makazi yake. Mtoto huyo amejulikana kwa jina la Jackson mtoto wa mzee Lyimo. Inaelezwa kuwa mtoto huyo alipotea tangu jana wakati akichunga mbuzi na wenzake,na hakuonekana hadi usiku huu majira ya saa moja alipokutwa ameuawa na kutupiwa kwenye karo la maji machafu yanayotoka kiwanda cha Jambo kilichopo katika kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga. Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia malunde1 blog kuwa mtoto huyo alikuwa anachunga mbuzi ndipo akatokea mwanamme huyo na kumnyonga shingo. Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya mtoto Happiness Kashinje mwenye umri wa miaka 9 kuuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika katika manispaa ya Shinyanga.
Malunde1 blog inaendelea kufuatilia tukio hili,tutakuletea taarifa kamili hivi punde.......
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin