Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIJANA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ZABUNI ZA SERIKALI.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo akitoa mafunzo kwa vijana na makundi maalum ukumbi wa Manispaa ya Songea akiwahimiza kutumia fursa zilizopo katika zabuni za umma Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo wapili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na vijana na makundi maalum baada ya mafunzo ya PPAA kukamilika. 


Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma 


Vijana na makundi maalum nchini wamehimizwa kutumia fursa zilizopo katika zabuni za umma kama njia ya kukuza biashara zao na kuongeza mchango wao katika uchumi wa Taifa. 


Wito huo umetolewa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Jumanne Mwankhoo, amesema uelewa wa sheria za ununuzi wa umma ni msingi muhimu kwa wafanyabiashara wanaotaka kushiriki kikamilifu katika zabuni za Serikali. 


Amesisitiza kuwa mfumo wa ununuzi wenye uwazi na ushindani unalenga kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi katika miradi ya maendeleo.


Mwankhoo amewataka PPAA na PPRA kuendelea kuhamasisha vijana na makundi maalum kutumia fursa zilizopo katika uwekezaji, biashara na uchumi bunifu, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza kipato kwa wananchi na kuimarisha uchumi wa nchi.


Kaimu Katibu Mtendaji wa PPAA, Pascal Kajuna, amesema mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ambapo hadi sasa wazabuni 1,717 na watumishi 705 wa idara za ununuzi na sheria wamefikiwa. 


Aidha, vijana 1,299 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamepewa mafunzo ya kuwawezesha kutambua na kudai haki zao katika michakato ya ununuzi wa umma




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com