Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wakala wa barabara za mijiini na vijijini (TARURA) inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya barabara nchini huku serikali ikiwa imetoa takribani ya fedha shilingi Milioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo yakiwemo madaraja ya mawe.
Akizungumza na Wanahabari Kwenye Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma mkoani dodoma mkuu wa kitengo na uhusiano kwa umma Tarura Catherine Sungura amesema Tarura tunahudumia barabara zenye urefu wa laki moja na 44 nchi nzima huku barabara za lami zikiwemo barabara za lami,mawe na udongo.
Tunaendelea kujenga Madaraja nchi nzima katika kuhakikisha jamii inapata huduma za maendeleo kupitia barabara hizo hivyo kufikia sasa tuna madaraja 490 .
" mwaka 2024, 2025 Tarura tulipokea fedha kutoka benki ya dunia takribani ya dola Milioni 65 katika kwenda kuboresha barabara ambazo ziliathirika na Mvua za Elnino ambapo kwa sasa tumerudisha Mawasiliano ya barabara hizo kwa asilimia 70 katika Vijiji,Wilaya na Mikoa." Amesema Mkuu wa kitengo sungura"
Aidha mameneja wa mikoa hususani mkoa wa tabora wilaya ya sikonge na urambo huduma zimerejea kwa wananchi kama kawaida hivyo tarura tunaendelea kuboresha miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa TACKTIC wa miji 45 ambapo tunajenga masoko, barabara za lami na Mradi wa DMDp 2 ambao tunajenga takribani kilomita 250 katika wilaya 5 za mkoa wa Dar esalaam.
Vilevile kwa mkoa wa Dar esalaam tuwatoe hofu Wananchi kuwa wakandarasi wamerejea kukamilisha miundombinu ya barabara hiyo hivyo Mtaa wa majohe kivule kuna kilomita 2 za barabara za zege na kigamboni.
Katika Hatua nyingine tarura tumetoa ajira kwa maafisa usafirishaji (bodaboda) mkoani morogoro wilaya ya ifakara na wanaenda kuinuka kiuchumi kupitia miradi hiyo ya barabara
Kwa upande wake afisa utumishi mkuu Speransia Mhapa ameongeza kuwa tarura imefanya mabadiliko mbalimbali kwenye sekta ya miundombinu nchini ambapo tunatambua katika maendeleo hayo watumishi wa umma wamekuwa na mchango mkubwa katika kukamilisha suala hilo la miundombinu.
Nitoe wito Kwa wananchi wote wanaoendelea kutembelea kwenye maadhimisho haya wafike kwenye banda la Tarura kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA).


Social Plugin