
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amefariki dunia leo Jumamosi, Juni 20, 2026, akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa akiendelea na matibabu.
Taarifa kuhusu kifo cha SACP Richard Abwao zimethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ambaye amesema kuondoka kwa kiongozi huyo ni pigo kubwa kwa Jeshi la Polisi na wananchi wa Mkoa wa Tabora kutokana na mchango wake mkubwa katika kudumisha usalama, amani na utulivu wa mkoa huo.
Mhe. Chacha ameeleza kuwa SACP Richard Abwao alikuwa mmoja wa viongozi waliotekeleza majukumu yao kwa weledi na kujituma, hali iliyomfanya kuheshimika ndani na nje ya Jeshi la Polisi.
Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ugonjwa wake pamoja na ratiba za mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia pamoja na mamlaka husika katika siku zijazo.
R.I.P SACP Richard Abwao.
Social Plugin