Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA SIASA YA CCM KATA YA KISHAPU YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA NA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI NA SHUGHULI ZINGINE

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kutembelea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kwenye Kata hiyo ikigusa sekta ya Elimu, Afya, Maji na uuzwaji wa pamba kwenye baadhi ya Amcos ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika kwa ufanisi na wananchi wanapata huduma bora huku utekelezaji wa maagizo ya serikali ukitekelezwa.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo Juni 30, 2026, Diwani wa Kata ya Kishapu, Mhe. Joel Ndettoson, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha miundombinu ya huduma za jamii, hatua inayochochea maendeleo ya wananchi na kuboresha maisha yao.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu, Paul Shagembe, pamoja na Katibu wa CCM Kata, Cornel Zengo, wamewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda na kutunza miradi hiyo ili iweze kudumu na kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Kamati ilikagua miradi mbalimbali ikiwemo:.

1- Ujenzi wa choo cha kisasa katika eneo la maegesho ya magari ya mnad wa Mhunze ulioko Kitongoji cha Mwasele "B" chenye jumla ya matundu matatu (3) pamoja na chumba cha mkusanya mapato.


2- Ujenzi wa matundu matano ya vyoo katika Shule ya Msingi Lubaga.


3- Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Serikali, ukiwa ni mfano wa ushirikiano utakaoleta matokeo makubwa shule ya msingi Mwabusiga



4- Mradi wa tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 50,000 litakalohudumia wananchi wa Mwabusiga
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Paul Shagembe


5- Mradi mkubwa wa BOOST katika Shule ya Sekondari Isoso

Kamati pia ilikagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi ndani ya Shule ya Sekondari Isoso unaotekelezwa kupitia fedha za Serikali Kuu chini ya Programu ya BOOST.

Mradi huo ulipokea jumla ya Shilingi 342,900,000 kwa ajili ya kujenga Vyumba sita vya madarasa ya shule ya msingi, Matundu 10 ya vyoo vya shule ya msingi, Vyumba viwili vya madarasa ya awali, Matundu sita ya vyoo vya shule ya awali, Jengo la utawala na Matundu mawili ya vyoo vya walimu.


Kazi za ujenzi zilianza rasmi Septemba 1, 2025 na kufikia Juni 30, 2026 miundombinu yote iliyopangwa ilikuwa imekamilika kwa asilimia 100 kupitia mfumo wa Force Account chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

Jumla ya Shilingi 340,995,000 tayari zimetumika, huku salio la Shilingi 1,905,000 likisubiri kulipwa kama retention baada ya kukamilika kwa taratibu za uthibitishaji wa kazi.


6- Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Isoso uliogharimu Shilingi 71,800,000 kupitia Programu ya BOOST.

Fedha hizo zilitumika kununua vifaa vya ujenzi, kugharamia nguvu kazi na matumizi mengine ya ujenzi. Mradi umekamilika kwa asilimia 100 na umeanza kutumika, huku wanafunzi 97 wa elimu ya awali wakianza kutumia madarasa hayo tangu Aprili 2026.

Uongozi wa shule umeeleza kuwa mradi huo umeondoa msongamano wa wanafunzi madarasani, umeboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kuongeza ari ya wazazi kuwapeleka watoto shule.

Pamoja na mafanikio hayo, changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ni pamoja na upatikanaji wa maji kwa shughuli za ujenzi na ucheleweshaji wa baadhi ya vifaa vya ujenzi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Cornel Zengo


maeneo yaliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na:.

-Eneo la kujenga Shule shikizi ya Lubaga lenye ukubwa wa ekari saba lililoko lisolyang'wale


-AMCOS ya Lubaga na Buluba Mhunze tawi la Mwabusiga ili kujionea hali halisi ya ununuzi na uuzaji wa zao la pamba ambapo wananchi wameonesha kuridhishwa na malipo kuwa ya haraka na papo kwa papo ukilinganishwa na hali ya kipindi kilichopita malipo kufanyika kwa njia ya benki jambo lililokuwa likichelewesha malipo yao na kungeza migogoro kwenye zao hilo.


- Kamati hiyo pia imetembelea Zahanati ya Lubaga ambapo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Christian Ngowi ameelezea mapungufu yaliyopo huku viongozi wa Cham ahicho na Diwani wa Kata wakiahidi kuzifikisha mahali husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuongeza ubora wa huduma za afya kwa wananchi.
Diwani wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson


Baada ya kukagua miradi yote, Kamati ya Siasa ya CCM Kata ya Kishapu imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya wananchi na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kwa usimamizi makini.


Pia Kamati imeshauri kuwepo na marekebisho kwenye baadhi ya miradi kwenye nyufa zilizoonekana kabla ya mradi kukabidhiwa huku wakiwataka wananchi kuendelea kushiriki katika ulinzi na utunzaji wa miradi hiyo ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Shadrack Machiya

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wazazi Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Edward Sengela
Mtendaji wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Catherine Kayombo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Isoso Annusiantha Audax akisoma taarifa ya mradi

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Isoso Girbert Mtunguja akisoma taarifa ya mradi
Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Lubaga Kata ya kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa kitongoji cha Lubaga Makaranga

Mhasibu Amcos ya Lubaga Juma Nyahigi
Mradi wa Matunzu 3 ya choo na Ofisi ya mkusanya
mapato mnada wa Mhunze




Shule ya Sekondari Isoso












Isoso Shule ya msingi




Picha ya Zahanati ya Lubaga










Picha Eneo la kujenga Shule shikizi ya Lubaga lililoko lisolyang'wale




Picha Matundu ya vyoo Lubaga






Picha ya Mradi wa maji ya Ziwa Viktoria Mwabusiga



Picha ya vyumba vya madalasa Mwabusiga






Picha za Amcos ya Lubaga






Picha ya Amcos ya Buluba Mhunze tawi la Lubaga











































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com