Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU

Yanga SC imejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026 baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa ligi uliopigwa leo, Juni 30, 2026. 

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 75, idadi iliyotosha kutangaza rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2025/2026. 

Katika michezo mingine ya leo, Simba SC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC, huku Fountain Gate FC na Singida Black Stars FC zikitoshana nguvu kwa sare ya mabao 2-2.

Namungo FC iliwashinda Mtibwa Sugar FC mabao 2-1, Coastal Union FC ikalazimishwa sare tasa ya 0-0 na Pamba Jiji FC, wakati Mashujaa FC na Tanzania Prisons nazo zikitoka sare ya bila kufungana. Mbeya City FC pia iligawana pointi na TRA United FC baada ya kutoka sare ya 0-0.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com