Na Dotto Kwilasa,Dodoma
WIZARA ya Viwanda na Biashara imewasilisha bungeni makadirio ya matumizi ya Shilingi bilioni 137.8 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, yakilenga kuendeleza sekta za viwanda na biashara pamoja na kuimarisha uchumi wa nchi.
Akiwasilisha makadirio hayo leo Mei 22, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 104.1 zimepangwa kwa matumizi ya kawaida, ikiwemo Shilingi bilioni 78.0 kwa mishahara ya watumishi na Shilingi bilioni 26.0 kwa matumizi mengine ya uendeshaji.
Aidha, amesema Shilingi bilioni 33.6 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku fedha zote za maendeleo zikitarajiwa kutoka katika mapato ya ndani ya Serikali.
Kwa mujibu wa Waziri Kapinga, bajeti hiyo inalenga kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuongeza kasi ya uzalishaji wa viwanda vya ndani, kukuza biashara pamoja na kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la ndani na la kimataifa.

Social Plugin