Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WATUMISHI wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wamepima afya na kushiriki michezo mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya Wellness Day, tukio lililolenga kuimarisha afya ya akili na mwili ili kuongeza ufanisi kazini na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Tukio hilo limefanyika Mei 2, 2026 katika viwanja vya michezo vya Fresho vilivyopo Manispaa ya Shinyanga, likiwakutanisha watumishi wa benki hiyo katika shughuli za michezo na elimu ya afya.
Mmoja wa watumishi hao, Donard Mgaya, amesema tukio hilo limewasaidia kujumuika pamoja, kujuana na kuchangamsha miili, hali inayowapa nguvu mpya ya kuendelea kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi.
“Wellness Day imetusaidia kukutana kama timu, kuimarisha afya zetu na kupata nguvu mpya ya kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi,” amesema Mgaya.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana, amesema michezo ina mchango mkubwa katika kuleta furaha kwa watumishi na kuongeza ufanisi kazini, huku akiishukuru benki hiyo kwa kuendelea kutekeleza programu hiyo muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi.
“Michezo huleta furaha kwa watumishi na kuongeza ufanisi kazini, ndiyo maana tunaendelea kuipa kipaumbele programu hii muhimu,” amesema Wagana.
Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Theophill Akaro, amewataka watumishi hao kutumia fursa hiyo kujijenga upya na kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi.
“Michezo na elimu ya afya ya akili ni nyenzo muhimu inayomfanya mtumishi kuwa na utulivu, hivyo tumieni fursa hii kujijenga upya na kuongeza bidii katika kazi,” amesema Akaro. Ameongeza kuwa maadhimisho ya Wellness Day yamekuwa sehemu ya utamaduni wa benki hiyo, yakilenga kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na afya bora ya mwili na akili, jambo ambalo ni msingi wa utoaji wa huduma bora za kifedha mkoani Shinyanga na Kanda ya Magharibi kwa ujumla.
TAZAMA MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Theophill Akaro akizungumza.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Theophill Akaro akizungumza.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza.
Mwakilishi wa Rasilimali watu Benki ya CRDB Veronica Muumba akizungumza.
Social Plugin