Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IPI YAWATEUA MABALOZI 500 WA KUITANGAZA AMANI NDANI NA NJE YA NCHI

Na Theophilida Felician 

Taasisi ya International Peace information (IPI) yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam imewateua mabalozi wa amani watakaofanya kazi yakuitangaza amani nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mei 5 2026 Rais wa Taasisi ya International Peace Information (IPI) Prof. Wilson George Munguza amesema kuwa taasisi hiyo ambayo imejikita zaidi kuhamasisha amani nchini imeendelea kutumia njia mbalimbali kuitangaza amani lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ili kuhakikisha amani ya nchi inakuwa tulivu na kudumu nyakati zote.

Rais Munguza amefafanua kuwa mabalozi hao miatano walioteuliwa kwa awamu ya kwanza wanaendelea kunolewa kwa muda wa miezi miwili ili kuongezewa mbinu na maarifa zaidi kwa lengo la kuwaweka sawa na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa na baada ya muda huo wanatarajia kuapishwa mnamo Tarehe 31 Julai 2026.

Aidha amesema taasisi imelenga kuwapeleka mabalozi katika nchi za Afrika mashariki hususani zenye kukabiliwa na migogoro ya ukosefu wa amani ikiwemo Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kwingineko.

Hata hivyo ameongeza kuwa licha ya kuwateua mabalozi tayari taasisi imewateua wabunge wa amani ambao wanaendelea kusaidiana majukumu na wabunge wa majimbo ambapo hivi karibuni taasisi imemtunuku tuzo ya pongezi spika wa bunge Mhe .Mussa Azzan Zungu ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi zake katika kuzisimamia vyema shughuli za bunge hilo tukufu.

Ameishukuru serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyoendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ambapo amewaomba viongozi wa wilaya, mikoa na wengine kuwapatia ushirikiano mabalozi wa amani watakapokuwa wameanza majukumu maeneo watakayopangiwa kote nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com