Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

USHIRIKI WA VIJANA NA WANAWAKE UIMARISHWE KATIKA UONGOZI WA VYOMBO VYA HABARI – IDDA MUSHI


Lusaka, Zambia

WADAU wa sekta ya habari barani Afrika wameendelea kujadili mustakabali wa tasnia hiyo katika Mkutano wa Africa Media Convention unaoendelea jijini Lusaka katika Ukumbi wa Mulungushi International Conference Centre.

Mkutano wa Africa Media Convention ni jukwaa la wanahabari na wadau wa vyombo vya habari barani Afrika linalolenga kuimarisha uandishi wa habari, uhuru wa vyombo vya habari na uendelevu wa sekta hiyo.
  
Katika mjadala wa rasimu ya Katiba ya AMC, Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Congress of African Journalists Asociation, CAJ anayetokana na chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania JOWUTA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tanzania Women Journalist Delegation, TWJD Bi Idda Mushi amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha ushiriki wa uhakika wa vijana na wanawake katika uongozi na maamuzi ya vyombo vya habari.

Bi Idda amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha vijana na wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika uongozi na maamuzi ya sekta ya habari ili kuimarisha uwakilishi na ufanisi wa sekta hiyo. 

Amesema ushiriki huo utaongeza uwakilishi na kuimarisha maamuzi yenye tija kwa maendeleo ya tasnia ya habari barani Afrika.

Aidha, ametoa wito kutiliwa mkazo wa utekelezaji wa vitendo wa Katiba ya AMC badala ya kuishia kwenye misingi ya maandishi pekee.

Mkutano huo wa AMC unaofanyika ana kwa ana na kwa njia ya mtandao (live stream) kupitia zoom, ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

AMC iliasisiwa kwa mara ya kwanza katika jiji la Arusha nchini  Tanzania na imeendelea kufanya mikutano katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Nigeria, Ghana, Morocco na mwaka huu nchini  Zambia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com