Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIMI NI SAMIA YULE YULE – RAIS SAMIA AVUNJA UKIMYA KUHUSU MABADILIKO



Na mwandishi wetu, Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa yeye ndiye yule yule na hajabadilika kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwenye Mitandao mbalimbali ya kijamii.

Rais Samia amesisitiza hayo leo Alhamisi Aprili 23, 2026 Ikulu ya Magogoni Jijini Dar Es Salaam, akibainisha kuwa bado yeye ni Kiongozi anayeamini katika maridhiano kama ilivyokuwa falsafa yake tangu wakati amechukua uongozi wa Nchi.

"Wakati nafuatilia uwasilishaji wa ripoti hii nilisikia sentensi inayosema 'Tunamtaka Samia wetu tunayemfahamu'- kanakwamba nilipoingia nilikuwa Samia mwingine na sasa ni Samia mwingine, nataka niwahakikishie watanzania kuwa mimi ni Samia yuleyule wa falsafa ya maridhiano (4R), ninachotaka ni ushirikiano wenu katika kutekeleza falsafa hiyo." Amesema Rais Samia.

Rais Samia pia amewasihi watanzania kutokubali kurubuniwa na kuchochewa na wanaharakati, wanasiasa na wenye maslahi binafsi katika kuharibu tunu ya amani ya Tanzania, akisisitiza ushirikiano wa pamoja katika kuijenga Tanzania ili amani na umoja uendelee kutamalaki.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com