Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WOTE TUNAOIPENDA TANZANIA TUPO UPANDE WA TUME YA JAJI CHANDE- SALUM MWALIMU



Na mwandishi wetu, Dar

Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amewakosoa vikali wale wanaopinga Ripoti ya Tume huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema wapo baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao nchi kuwa tulivu na yenye amani ni hasara kwao kutokana na kufaidika na migawanyiko na ukosefu wa amani.

Mwalimu ambaye pia alikuwa Mgombea wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kupitia CHAUMMA, ametoa kauli hiyo leo Aprili 23, 2025, muda mfupi baada ya Tume ya Jaji Mstaafu Mohamed Othman Chande kuwasilisha ripoti hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema ripoti hiyo na hotuba ya Rais Samia imejibu kikamilifu baadhi ya dosari zilizokuwa zinasemwa.

"Kuleta matumaini ni mapokeo, kuna wengine hawapendi tu na utulivu na amani ya nchi wao kwao ni hasara lakini kwa yeyote ambaye kwakweli ana nia njema na nchi hii, ameisikiliza ripoti, ameona weledi wa tume na uzoefu wao na uzuri mwenye ripoti yake tumemsikia anasema tuungane tutekeleze haya ya Tume- inakuwaje wewe unakuja tena unasema chokochoko?"

"Kila mwenye kufikiri, kila mwenye kuitakia mema nchi yetu na kila mwenye kujutia na kile kilichotokea Oktoba 29 na hataki tena ijirudie, mimi ninaamini ataungana na Tume, ataungana na Mhe. Rais Samia na sasa ebu kama ni kuhukumiana, tuanze kuhukumiana kwenye utekelezaji wa yale tuliyoahidiwa siku ya leo." Amesisitiza Salum Mwalimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com