Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS YAWATAKA WAZALISHAJI WA MKAA MBADALA KUZINGATIA VIWANGO


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa wajasiriamali wanaozalisha nishati safi ya kupikia, hususan mkaa mbadala, mkoani Kigoma kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango.

Mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia wazalishaji hao kuboresha ubora wa mkaa mbadala wanaozalisha ili uweze kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Viwango wa TBS, Bw. Spiradson Kagaba, amesema matumizi ya mkaa mbadala yana faida nyingi ikiwemo kupunguza taka, kutotoa moshi unaodhuru afya, kuwaka kwa muda mrefu na kusaidia kulinda uoto wa asili kwa kupunguza ukataji wa miti.

Amesema kuwa matumizi ya nishati hiyo ni hatua muhimu katika kulinda mazingira na kuboresha afya za watumiaji wa nishati za kupikia.

Aidha, wazalishaji hao wametakiwa kuzingatia viwango vilivyowekwa ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa, kulinda afya za watumiaji na kuhifadhi mazingira.

“Hatua hii inaunga mkono mkakati wa Serikali wa kupunguza ukataji wa miti na kuhamasisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira,” amesema Kagaba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com