Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LUKUMAY AWAHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA MBUNGE ATAKAYECHAGULIWA NA KUACHANA NA MAKUNDI


Aliyekuwa mtia nia wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elias Lukumay akifanyiwa maombi na viongozi wa dini
Na Woinde Shizza, Arusha

Aliyekuwa mtia nia wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elias Lukumay, ameushangaza umma baada ya kuandaa sherehe kubwa ya kuushukuru uongozi wa chama na wananchi wa jimbo hilo licha ya jina lake kutoorodheshwa katika hatua ya mwisho ya mchujo wa wagombea.
Akizungumza nyumbani kwake Agosti 24, 2025 mbele ya mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge mteule wa jimbo hilo Johannes Lukumay, mabalozi wa nyumba kumi na wenyeviti wa vitongoji, Lukumaye alisema amefanya sherehe hiyo kama ishara ya kuthamini mshikamano, heshima na upendo alioupata wakati wa safari yake ya kisiasa.
“Mahaba haya na mapenzi mliyoonyesha juu yangu sina cha kuwalipa ,Mlinipa ushirikiano mkubwa, lakini kwa bahati mbaya jina langu halikurudi ,Nimeona niwashukuru kwa kuungana nami leo,” alisema Lukumaye.
Aidha Lukumaye alisema dhamira yake haikuwa tu kushinda ubunge, bali kusaidia wananchi wa kata zote 27 za Arumeru Magharibi kushughulikia changamoto zinazowakabili, ikiwemo umasikini na ukosefu wa elimu bora.
Kwa upande wa mgombea ubunge wa Jimbo hilo Johannes Lukumay Alifichua kuwa azma yake kubwa ni kuondoa umasikini kwa kuanzisha mfuko maalum wa elimu utakaosaidia watoto wanaotoka katika familia duni kupata nafasi ya kusoma bila changamoto za ada.

“Nilipokuwa nasoma shule ya msingi nilitembea bila viatu kwa miaka saba, na nilivaa viatu nilipoingia sekondari. Ndio maana nachukia umasikini. Kwa sasa nasomesha watoto 89 wasioweza kununua hata daftari. Nimepania kuhakikisha kila mtoto wa Arumeru anasoma bila kikwazo cha ada,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, ambapo burudani, vyakula na vinywaji vilitolewa, hali iliyoongeza shamrashamra na kuonyesha mshikamano wa kijamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com