Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TISEZA KURATIBU UWEKEZAJI WA TRILIONI 10 KWALA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo; Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati; Menejimenti ya TISEZA pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo Kongani ya Viwanda ya Kwala pamoja na kutatua changamoto, ziara hiyon imefanyika leo Desemba 10, 2025 Mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo; Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati; Menejimenti ya TISEZA wakikagua maendeleo ya Kongani ya Viwanda ya Kwala, Mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari.

..........

Serikali kupitia Wizara mbalimbali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), imejipanga kuratibu uwekezaji wa viwanda 200 vyenye thamani ya shilingi trilioni 10, hatua inayotarajiwa kuleta manufaa kwa Taifa ikiwemo kuzalisha ajira 100,000.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo; Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati; Menejimenti ya TISEZA pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge kutembelea Kongani ya Viwanda ya Kwala kwa lengo la kukagua maendeleo ya viwanda na kutatua changamoto zilizopo.

Akizungumza katika ziara hiyo leo, Desemba 10, 2025, katika Halmashauri ya Kibaha mkoani Pwani, Prof. Mkumbo amesema kuwa kwa sasa kuna viwanda 20 vinafanya kazi ambayo vimetoa ajira Kwa watu 2,000, huku akieleza kuwa lengo ni kufikisha viwanda 200 vitakavyotoa ajira 100,000.

Prof. Mkumbo amebainisha kuwa hadi sasa wawekezaji wamewekeza shilingi bilioni 625 na wanatarajia kuongeza uwekezaji hadi kufikia shilingi trilioni 10.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com