MBOWE AMPONGEZA FATMA KARUME KUWA RAIS WA TLS

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amempongeza Fatma Karume kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa TLS.


“Ushindi wako umetuma ujumbe kuwa mawakili wa Tanganyika wanajua msimamo wako na wanaamini kwa dhati kuwa kwa kushirikiana na viongozi wenzako mliochaguliwa kuongoza TLS utawavusha katika kipindi hiki ambacho Taifa linapitia na kushuhudia majaribu mengi ya uvunjifu wa Katiba, sheria na kanuni mbalimbali.


"Umepokea kijiti katika wakati ambao mtangulizi wako (Tundu Lissu) yuko hospitalini baada ya jaribio la shambulizi lililolenga kumuua kushindikana.


“Tukutie moyo kuwa CHADEMA kama taasisi ya kisiasa tukiwa wadau wa masuala ya haki, sheria na utawala bora tuko nawe na tutaendelea kukupa ushirikiano wakati wote wa uongozi wako, wewe na wenzako wote.” -Mbowe 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527