BAADA YA NANDY NA BILLNAS......DIAMOND NA HAMISA MOBETTO WATUPIA VYA MAHABA MTANDAONI

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amerudi upyaa Kwenye headlines baada ya video zake za mahaba na Baby mama wake msanii Hamisa Mobetto kusambaa mtandaoni siku ya jana.





Jana Diamond na Hamisa wameonekana pamoja katika chumba kimoja huku wakikumbatiana na kushikana kitendo kilichoibua maswali mengi kwani kiukweli haijajulikana kama wapo pamoja au ni kiki.



Hii imetokea ikiwa ni wiki mbili tangu wawili hao walipokutana live kwenye Tuzo za SZIFF pale Mlimani City Dar ambapo Diamond alimkumbatia mwanamama huyo na kupigana mabusu motomoto mbele ya umati uliofika kushuhudia tukio la tuzo hizo.

Ni siku  chache tu video ya mahaba kati ya Nandy na Bill Nas ilizagaa mtandaoni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527