MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA USANDA - SHINYANGA



Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nshoma Shija (70) mkazi wa Kitongoji cha Mabu,kijiji cha Shabuluba kata ya Usanda  tarafa ya Samuye wilaya ya Shinyanga (Vijijini) mkoa wa Shinyanga ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

Malunde1 blog imeambiwa kuwa mwanamke huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake wakati anapika viazi nje ya nyumba yake majira ya saa moja usiku huu Jumamosi Aprili 21,2018. 

Inaelezwa kuwa mtu/watu wasiojulikana walimvamia mwanamke huyo kisha kumkata kwa kitu chenye makali shingoni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema wanafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwakamata wahusika wa mauaji hayo.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527