MSEMAJI WA SERIKALI : TUNDU LISSU BADO NI MGONJWA,SERIKALI HAIONI BUSARA KULUMBANA NAYE


Mkurugenzi Mkuu-Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu, Dkt Hassan Abbas amesema kwamba Tundu Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa.


Dkt Abbasi ameeleza kuwa, kwa sasa serikali bado inaendelea kumuombea mbunge huyo ili aweze kupona haraka.


Maneno hayo yametolewa ikiwa ni muda mfupi tangu Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alipozungumza na waandushi wa habari akiwa Hospitalini jijini Nairobi na kuituhuma serikali kuhusu masuala mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.


Miongoni mwa mambo mengi ambayo Tundu Lissu ameituhumu serikali ni pamoja na jaribio la kutaka kumuua lililotokea Septemba 7 mjini Dodoma, ambapo Lissu amesema licha ya kuwa miezi minne imepita tangu aliposhambuliwa kwa lengo la kuuawa, hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyekemea tukio hilo.


Lissu ameelekeza malalamiko yake pia kwa Bunge ambapo amekosoa uamuzi wa Bunge kukataa kugharamia matibabu yake, na kuacha mzigo wote kwa chama na familia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527