Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA SHINYANGA MJINI GEORGE KITALAMA AFARIKI DUNIA



George Kitalama enzi za uhai wake

Habari zilizotufikia hivip punde zinasema kuwa kada wa Chadema Mhe.George Kitalama amefariki dunia ghafla mjini Shinyanga jioni hii Jumapili Oktoba 8,2017.



Mhe Kitalama amewahi kuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya Shinyanga Mjini kuanzia mwaka 2014 hadi mwanzoni mwa mwaka 2017 na aliwahi kuwa Diwani Kata ya Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2010 -2015.

Inaelezwa kuwa alianguka akiwa kwenye kwenye kikao cha kamati ya mipango,miradi na afya ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika Wa Ebeneezer Kanisa Kuu Shinyanga Mjini.

Alipoanguka alikimbizwa hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga ambako ndiyo umauti umemkuta.


R.I.P Kitalama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com