WANAVIJIJI WILAYANI IKUNGI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MIRADI YA MAENDELEO


Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu (aliyesimama) amezindua awamu ya pili ya mradi wa kuwajengea wananchi uwezo ili kuibua na kuendeleza miradi ya maendeleo katika vijiji vyao wilayani humo.

Katika uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu alilipongeza shirika la HAPA kwa kusimamia vyema awamu ya kwanza ya mradi huo na hivyo kufanikisha kupata ufadhiri wa awamu ya pili ya mradi ambapo Vijiji 15 wilayani Ikungi vitanufaika.

Mhe.Mtaturu aliwata wasimamizi wa mradi huo kuendelea kusimamia vyema shughuli za mradi huo jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa miradi mingine kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Ikungi.

Mkurugenzi wa shirika la HAPA, Makyao Noel alisema Vijiji 10 wilayni Ikungi vilifikiwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo na hivyo kusaidia wananchi kuibua miradi 26 ya maendeleo na kwamba miradi miradi 12 ilikuwa ya maji, Zahanati, Vituo vya Afya, barabara pamoja na nyumba za watumishi na kwamba awamu ya pili ya mradi huo itavifikia Vijiji 15 wilayani Ikungi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, akitoa neno la shukurani kwenye uzinduzi huo uliokwenda sambamba na kujadili mafanikio na changamoto za mradi wa awamu ya kwanza ili kusaidia uboreshaji kwenye utekelezaji wa mradi wa pili utakaodumu kwa miezi sita kuanzia mwezi huu
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo
Aliyesimama ni Mkurugenzi wa shirika la HAPA, Makyao Noel alisema, akitoa ufafanuzi kwenye uzinduzi huo
Viongozi mbalimbali meza kuu

Wawezeshaji wa mradi
Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiwemo madiwani wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi huo
Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi huo

BMG Habari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527