WABUNGE WA UPINZANI WAIMBA WANA IMANI NA MKAPA, KIKWETE WAKIWA BUNGENI RAIS MAGUFULI AKIPOKEA RIPOTI YA MCHANGA WA MADINI


Bunge limezizima kwa makofi baada ya hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani.Wabunge wa upinzani ndiyo wengi waliobaki ukumbini baada ya wengi kwenda kufuatilia ripoti ya kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.


Wabunge wamesimama na kuanza kuimba huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wametajwa.


"Tuna imani na Mkaaapa...oya oya oya
Mkapa kweeeli...kweli
Kweli, kweli, kweli Mkapa.


Tuna imani na Kikweeetee...oya oya oya
Kikwete kweeli
Kweli, kweli, kweli Kikwete."


Wimbo huo umeimbwa baada ya Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kulitaka Serikali kuileta bungeni mikataba yote ya madini ili ijadiliwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments