WAZIRI MWAKYEMBE AWATAKA WASANII TANZANIA WAACHE KUIMBA MASUALA YA SIASA



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe amewasihi watanzania kuacha kutumiwa na viongozi mbalimbali kwa kuimba nyimbo za masuala ya kisiasa na badala yake wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata mafanikio.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya wizara yake.

"Tembea dunia kote huko, nimekwenda Nigeria na kuona wasanii wakubwa kama Tiwa Savage, Don Jazz, Akon, P Square wale hawaimbi kuhusu viongozi wao wa kisiasa.

"Hivyo niwasihi wasanii wangu, muache kuimba kuhusu siasa sababu hii ni ‘entertainment industry’ (sekta ya burudani) na sio ya masuala ya kisiasa, "alisema Waziri Mwakyembe.

Aidha, waziri alisema kama kuna msanii yeyote anayetaka kuwa mwanasiasa aache muziki akagombee udiwani kwani wasanii waliotaka kuchanganya siasa na muziki walipotea kabisa.

==>Msikilize hapo chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527